top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dr.Sospeter Mangwella, MD

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Umri wa kuonekana kwa dalili za selimundu

Jibu kwa ufupi


Swali la mteja: "Samahani dokta, sickle cell inaweza kuanza kutoa dalili mtoto akiwa mkubwa kama miaka nane?"


Jibu kwa ufupi: Ndiyo, inawezekana. Mtoto mwenye maumivu ya mifupa ya mara kwa mara, upungufu wa damu au macho ya njano apimwe selimundu. Soma Selimundu.



Maelezo


Kwa nini dalili huchelewa


  • Aina ya selimundu – HbSS na HbSβ⁰ ni kali, huanza mapema; HbSC na HbSβ⁺ ni nyepesi, huchelewa.

  • HbF ya juu – baadhi ya watoto hubaki na hemoglobini ya utotoni kwa wingi.

  • Dalili kutotambulika – maumivu, uchovu na homa za mara kwa mara hudhaniwa ni malaria au 'maumivu ya kukua'.

  • Mazingira – maji ya kutosha, kinga dhidi ya maambukizi na malaria hupunguza mashambulio.


Dalili kwa mtoto mkubwa


  • Maumivu ya mifupa, kifua au tumbo yanayojirudia.

  • Upungufu wa damu, uchovu, macho ya njano.

  • Maambukizi ya mara kwa mara.

  • Kuchelewa kukua au kubalehe.

  • Vidonda vya miguu, kukojoa kitandani (figo hushindwa kukaza mkojo).


Nini cha kufanya


  • Pima Hb electrophoresis (au HPLC) – si 'sickling test' pekee.

  • Mtoto akigundulika – kliniki ya selimundu: penicillin ya kinga, folic acid, kinga ya malaria, chanjo zote, hydroxyurea kwa ushauri.

  • Kunywa maji mengi, epuka baridi kali na uchovu mkubwa.

  • Ndugu wapimwe pia; wazazi wajue hali zao kabla ya kupanga watoto wengine.


Dalili za hatari


Hospitali mara moja ukiona:


  • Homa 38.5°C au zaidi.

  • Maumivu makali yasiyopungua kwa dawa za nyumbani.

  • Kupumua kwa shida, maumivu ya kifua.

  • Tumbo upande wa kushoto kuvimba ghafla, weupe mkubwa (wengu kujaa damu).

  • Udhaifu upande mmoja wa mwili, kushindwa kuongea, degedege.

  • Uume kusimama kwa maumivu zaidi ya saa 2.


Lini umwone daktari


  • Maumivu ya mifupa ya mara kwa mara.

  • Upungufu wa damu usioisha kwa madini chuma – soma Upungufu wa damu wa madini chuma.

  • Macho ya njano yanayojirudia.

  • Historia ya selimundu kwenye familia.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Selimundu inaweza kuanza kuonyesha dalili akiwa na miaka 8?

Ndiyo, hasa aina nyepesi.

2. Dalili za kwanza za selimundu ni zipi?

Mara nyingi mikono au miguu kuvimba na kuuma, miezi 6 hadi miaka 2.

3. Kipimo gani kinathibitisha selimundu?

Hb electrophoresis au HPLC.

4. Mtoto wangu ana sickle trait, ataugua?

Kwa kawaida hapana; ni mbebaji tu.

5. Selimundu inatibika?

Inadhibitika vizuri kwa huduma ya kliniki; upandikizaji wa uloto unaweza kuponya baadhi.

6. Folic acid inatibu selimundu?

Hapana, husaidia utengenezaji wa damu tu.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 17:07:30

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

  2. Piel FB, Steinberg MH, Rees DC. Sickle cell disease. N Engl J Med. 2017;376(16):1561–73.

  3. National Heart, Lung, and Blood Institute. Evidence-based management of sickle cell disease: expert panel report. Bethesda: NIH; 2014.

bottom of page