top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Vichomi ukeni vya kuja na kupotea kwenye ujauzito wa miezi 9: Sababu na njia za kuthibiti nyumbani

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Badilisha mkao, pumzika, tembea polepole, kuoga maji ya uvuguvugu. Vichomi vya mpangilio vinavyokaribiana, damu, maji kutoka au mtoto kupunguza kucheza – hospitali. Soma Dalili za awali za uchungu.


Maelezo


Visababishi vya kawaida


  • Kichwa cha mtoto kubana neva.

  • Mtoto kujigeuza.

  • Mishipa ya mfuko kuvutika.

  • Mlango wa kizazi kulainika.


Visababishi vya kuchunguza


  • Uchungu – mikazo ya mpangilio.

  • UTI – kuchoma kukojoa.

  • Maambukizi ya uke – muwasho, uchafu.

  • Damu – soma Tone la damu wakati wa mimba.


Nini cha kufanya


  • Lala kwa ubavu; mto kati ya magoti.

  • Tembea polepole; epuka kusimama muda mrefu.

  • Mazoezi ya nyonga (kutikisa nyonga kwa mikono na magoti).

  • Maji ya uvuguvugu – si moto sana.

  • Pumua taratibu wakati wa kichomi.

  • Fuatilia mtoto kucheza – soma Kucheza kwa mtoto tumboni.


Dalili za hatari


Hospitali mara moja ukiwa na:


  • Mikazo ya mpangilio kila dakika 5 au chini.

  • Damu au maji kutoka.

  • Homa, kuchoma kukojoa.

  • Mtoto kupunguza kucheza.

  • Maumivu makali yasiyokoma.


Lini umwone daktari


  • Vichomi vinavyokuzuia kutembea au kulala.

  • Muwasho au uchafu ukeni.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Vichomi ukeni mwezi wa 9 ni kawaida?

Ndiyo, mara nyingi.

2. Ni dalili ya uchungu?

Huweza kuwa, kama vina mpangilio na vinakaribiana.

3. Nifanye nini?

Badilisha mkao, pumzika, maji ya uvuguvugu.

4. Husababishwa na nini?

Kichwa cha mtoto kubana neva na mlango kulainika.

5. Lini ni hatari?

Damu, maji, homa, mtoto kupunguza kucheza.

6. Naweza kutumia dawa?

Paracetamol kwa ushauri; epuka NSAID.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:15

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Cunningham FG, et al. Williams Obstetrics. 26th ed. New York: McGraw-Hill; 2022.

  2. National Institute for Health and Care Excellence. Intrapartum care (NG235). London: NICE; 2023.

  3. World Health Organization. WHO recommendations on antenatal care for a positive pregnancy experience. Geneva: WHO; 2016.

bottom of page