top of page

Dalili na viashiria vya magonjwa mbalimbali

Unashauriwa kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala. Bofya picha au neno soma zaidi ili kuingia kwenye makala kwa undani.

Kukojoa mara kwa mara

Kukojoa mara kwa mara

Kukojoa mara kwa mara ni kukojoa zaidi ya mara 8 kwa siku au kuamka usiku zaidi ya mara moja kukojoa. Ni muhimu kutofautisha: kukojoa mkojo mwingi kila mara (kunywa maji mengi, kisukari, dawa za kutoa maji) na kukojoa kidogo kidogo mara nyingi (UTI, tezi dume, kibofu kuwa nyeti, ujauzito, kichocho). Kukojoa sana pamoja na kiu kali na kupungua uzito huashiria kisukari; pamoja na maumivu na kuungua – UTI.

Kukojoa mara kwa mara usiku (nocturia)

Kukojoa mara kwa mara usiku (nocturia)

Kukojoa usiku (nocturia) ni kuamka zaidi ya mara moja usiku kukojoa. Huongezeka na umri. Visababishi vikuu ni kunywa maji, chai au pombe jioni, tezi dume kukua, kibofu kuwa nyeti, kisukari, moyo kushindwa (maji ya miguuni hurudi kwenye damu ukilala), figo, sleep apnoea (kukoroma) na dawa za kutoa maji zinazomezwa jioni. Huharibu usingizi na huongeza hatari ya kuanguka kwa wazee.

Kukojoa kwa shuruti (urgency)

Kukojoa kwa shuruti (urgency)

Kukojoa kwa shuruti (urgency) ni hamu ya ghafla na kali ya kukojoa ambayo ni vigumu kuizuia, wakati mwingine mkojo ukitoka kabla ya kufika chooni. Mara nyingi husababishwa na UTI (pamoja na kuungua), kibofu kuwa nyeti (overactive bladder), tezi dume, mawe ya kibofu, kichocho, interstitial cystitis, na magonjwa ya neva (kiharusi, uti wa mgongo, kisukari). Kahawa, pombe na vinywaji vya soda huzidisha.

Mkojo kutoka wenyewe

Mkojo kutoka wenyewe

Mkojo kutoka wenyewe (urinary incontinence) ni kushindwa kuzuia mkojo. Aina kuu ni: kuvuja ukikohoa, kucheka au kunyanyua (stress – misuli ya nyonga dhaifu baada ya kujifungua au komahedhi); kuvuja kwa hamu ya ghafla (urge – kibofu nyeti); kuvuja kidogo kidogo kwa kibofu kujaa (overflow – tezi dume, neva); na kuvuja mfululizo mchana na usiku (fistula baada ya uzazi pingamizi). Kuna matibabu – mazoezi ya nyonga, mazoezi ya kibofu, dawa na upasuaji.

Kukojoa kitandani kwa mtu mzima

Kukojoa kitandani kwa mtu mzima

Kukojoa kitandani kwa mtu mzima (nocturnal enuresis) si kawaida na mara nyingi kuna chanzo kinachotibika: kibofu nyeti, tezi dume kubwa (kibofu kujaa na kuvuja), kisukari, UTI, sleep apnoea, pombe nyingi, dawa za usingizi, degedege usiku (kifafa) na matatizo ya neva. Wachache wameendelea tangu utotoni. Kukojoa kitandani kulikoanza ghafla ukubwani kunahitaji uchunguzi.

bottom of page