top of page

Dalili na viashiria vya magonjwa mbalimbali

Unashauriwa kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala. Bofya picha au neno soma zaidi ili kuingia kwenye makala kwa undani.

Mapigo ya moyo kwenda taratibu zaidi (bradycardia)

Mapigo ya moyo kwenda taratibu zaidi (bradycardia)

Mapigo ya moyo kwenda taratibu kwa lugha ya kitiba hufahamika kama bradycardia. Bradycardia ni hali ya mapigo ya moyo kuwa chini zaidi ya kiwango cha kawaida, yaani yaliyo chini ya midundo 60 kwa dakika (60b/min). Mapigo ya moyo ya kawaida kwa mtu mzima huwa kati ya midundo 60 hadi 100 kwa dakika, na chini ya 60 kwa watu wanariadha waliofunzwa na wanaofanya mazoezi yenye mpango maalumu.

Moyo kwenda kasi

Moyo kwenda kasi

Moyo kwenda kasi kitiba hufahamika kama tachycardia, hii ni hali ya kuhisi moyo unakwenda kwa kasi Zaidi ya kawaida. Kwa kawaida mapigo ya moyo huhesabiwa kwa kuhesabu midundo ya mishipa ya damu au kuhesabu midundo ya moyo. Endapo midundo ya moyo imezidi kiwango cha mapigo 100 kwa dakika mtu husemekana kuwa ana tatizo la tachycardia.

Kuhisi mapigo ya moyo

Kuhisi mapigo ya moyo

Hisia za mapigo ya moyo huitwa kitiba kwa jina la 'palpitation', hii ni hali ya kuhisi moyo unakwenda taratibu au kwa kasi zaidi ya kawaida. Hisia za mapigo ya moyo huweza kusababishwa na mambo ya kawaida ambayo huhitaji kuwa na hofu nayo au kumaanisha tatizo la moyo linalohitaji kufanyiwa uchunguzi wa haraka, hata hivyo mara nyingi hisia za mapigo ya moyo huwa hazisababishwi na mambo ya hatari.

Fangasi kwenye ulimi na kinywa

Fangasi kwenye ulimi na kinywa

Maambukizi ya fangasi kwenye ulimi hufahamika kitiba kwa jina la oral thrush au oral candidiasis, maambukizi haya husababishwa na fangasi wanaoitwa candida albicans. Fangasi huyu makazi yake ni ndani ya mdomo ya binadamu, hata hivyo kuna baadhi ya sababu zinaweza kusababisha fangasi kuongezeka maradufu kisha kusababisha mwonekano wa dalili za maambukizi kwenye midomo na ulimi.

Udhaifu wa umbile la kichwa cha mtoto- Kraniosinostosisi

Udhaifu wa umbile la kichwa cha mtoto- Kraniosinostosisi

Kraniosinostosisi ni tatizo la kuzaliwa linalosababishwa na kufunga mapema kwa mishono ya fuvu na linaweza kubadilisha umbo la kichwa cha mtoto. Utambuzi wa mapema, ufuatiliaji wa ukuaji na matibabu yanapohitajika husaidia mtoto kupata nafasi nzuri ya ukuaji wa kawaida na maisha yenye afya.

bottom of page