top of page

Elimu ya magonjwa kwa mjamzito

Sehemu hii utajifunza maelezo ya ziada kuhusu matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa ujauzito. Unashauriwa siku zote kuwasilaina na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile iliyoandikwa humu ili kupata ushauri unaoendana na hali yako ya kiafya.

Namna sahihi ya kusukuma mtoto

Namna sahihi ya kusukuma mtoto

Kuvuta pumzi kwa kina ni jambo la kwanza linachotakiwa ili kusaidia juhudi za kusukuma mtoto. Kwenye hatua ya pili ya leba (uchungu) utatakiwa kusukuma mtoto ili aweze kutoka kirahisi, kumbuka ili kupata nguvu zenye ufanisi, unatakiwa kuvuta pumzi kwa kina kiasi na si kwa kina sana.

Kuandaa nyonga kabla ya kujifungua

Kuandaa nyonga kabla ya kujifungua

Wakati wa kujifungua unapokaribia, mtoto atashuka chini ya tumbo kuelekea kwenye shimo la nyonga katika pozi la kichwa chini matako juu. Jukumu lako kubwa ni kujiweka fiti kimwili ili kumwezesha mtoto apite kirahisi kwenye nyonga na tundu la uzazi.

Namna ya kulala pozi la kiafya unapolala chali kwa mjamzito

Namna ya kulala pozi la kiafya unapolala chali kwa mjamzito

Baada ya miezi minne ya kwanza ya ujauzito, kulalia mgongo kwa muda mrefu kunatakiwa
kuepukwa, hii ni kwa sababu uzito wa mtoto na mfuko wa uzazi hugandamizi mishipa mikubwa
ya damu

Namna ya kuamka unapotoka pozi la kukaa kwa mjamzito

Namna ya kuamka unapotoka pozi la kukaa kwa mjamzito

Unapokuwa umelala au kukaa chini, ni lazima uamke ili kusimama. Kumbuka kuamka kama
inavyoshauriwa kiafya

Pozi sahihi la kukaa kwa mjamzito

Pozi sahihi la kukaa kwa mjamzito

Ukiwa umekaa kwenye kiti hakikisha mgongo unagusa kiti na umekaa karibu na meza ,usiache nafasi kati ya mgongo na kiti na pia kuwe na nafasi ndogo kati ya tumbo na meza kama inavyoonekana kwenye picha

bottom of page