Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, MD
Dkt. Sospeter M, MD
Jumatatu, 21 Machi 2022
Boga mwitu
Boga mwitu ni tunda linalotokana na mimea ya matunda inayopatikana kwenye familia Cucurbitaceae . tunda hili huandaliwa kwa kupikwa na kutumika kama chakula.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Boga Mwitu
Mafuta
Madini
Sukari
Nyuzilishe
Protini
Vitamini
Kabohaidreti
Maji
Kemikali muhimu inayopatikana kwenye Boga mwitu
Kemikali muhimu inazopatikana kwenye boga mwitu ni pectin.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Boga mwitu lenye gramu 100
Nishati = 45kcal
Mafuta = 0.1g
Maji = 86.41g
Kabohaidreti = 12g
Sukari = 2.2g
Nyuzilishe = 2g
Protini = 1g
Vitamini zinazopatikana kwenye Boga mwitu lenye gramu 100
Vitamini A = 532mcg
Vitamini B1 = 0.1mg
Vitamini B2 = 0.02mg
Vitamini B3 = 1.2mg
Viatmini B5 = 0.4mg
Vitamini B6 = 0.154mg
Vitamini B9 = 27mcg
Vitamini C = 21mg
Vitamini E = 1.44mg
Vitamini K = 1.1mg
Madini yanayopatikana kwenye Boga mwitu lenye gramu 100
Kalishiamu = 48mg
Kopa = 0.07mg
Madini Chuma = 0.07mg
Magineziamu = 34mg
Manganaizi = 0.202mg
Fosifolasi = 33mg
Potashiamu = 352mg
Sodiamu = 4mg
Zinki = 0.15mg
Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Boga mwitu
Kusaidia kuboresha afya ya macho Pamoja na kuzuia magonjwa ya macho yatokanayo na uzee.
Kusaidia wagonjwa wa kisukari kwa kushusha kiwango cha sukari na kuweka msawazo
Kuimarisha utendaji kazi wa moyo na kuweka msawazo wa shinikizo la Damu mwilini.
Kulainisha choo na kusaidia kwa watu wenye tatizo la kupata choo kigumu
Kupunguza uzito
Imeboreshwa,
21 Machi 2022 15:58:52
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Squash. https://www.nutritionvalue.org/Squash%2C_raw%2C_butternut%2C_winter_nutritional_value.html?size=100+g. Imechukuliwa tarehe 10 January 2022.
Saavedra, M. J. , Aires, A. , Dias, C. , et al. Evaluation of the potential of squash pumpkin by‐products (seeds and shell) as sources of antioxidant and bioactive compounds. Journal of Food Science and Technology, 52(2), 1008–1015. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7382094/. Imechukuliwa tarehe 10 January 2022.
Armesto J, Rocchetti G, Senizza B, et al . Nutritional characterization of Butternut squash (Cucurbita moschata D.): Effect of variety (Ariel vs. Pluto) and farming type (conventional vs. organic). Food Res Int. 2020 Jun;132:109052. doi: 10.1016/j.foodres.2020.109052. Epub 2020 Feb 3. PMID: 32331650. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/32331650/. Imechukuliwa tarehe 10 January 2022.