top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Sima A, CO

Dkt. Charles W, MD

Ijumaa, 10 Aprili 2020

Faida za Alizeti mwilini
Faida za Alizeti mwilini

Mmea wa alizeti hutoa mbezu za alizeti zinazotumika kutengeneza mafuta mazuri yasiyo na kihatarishi kikubwa cha kupata magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.


Mbegu ya alizeti huwa na vitamini E, madini ya kopa, manganezi, seleniamu kwa wingi na mafuta ya omega 3 kwa wastani pamoja na virutubisho vingine ambavyo ni;


 • Vitamin A, C, D,K, B1, B2,B3, B5, B6, B12,

 • Madini ya Folate, cholini, Fosforasi,

 • Madini ya kolini

 • Wanga


Viinilishe vinavyopatikana kwenye mbegu za alizeti


 • Kabohaidreti

 • Nyuzilishe

 • Sukari

 • Maji

 • Mafuta

 • Protini

 • Vitamini

 • Maji


Viinilishe vinavyopatikana kwenye mbegu za alizeti zenye gramu 100


 • Nishati = 584kcal

 • Protini = 20.78g

 • Sukari = 2.62g

 • Mafuta = 51.46g

 • Nyuzilishe = 8.6g

 • Kabohaidreti = 20g

 • Maji = 4.7g


Vitamini zinazopatikana kwenye mabegu za alizeti zenye gramu 100


 • Vitamini B1 = 1.48mg

 • Vitamini B2 = 0.355mg

 • Vitamini B3 = 8.335mg

 • Vitamini B5 = 1.13mg

 • Vitamini B6 = 1.345mg

 • Vitamini B9 ­=227mcg

 • Vitamini C = 1.4mg

 • Vitamini E = 35.17mg


Madini yanayopatikana kwenye mbegu za alizeti zenye gramu 100


 • Kalishiamu = 78mg

 • Potashiamu = 645mg

 • Madini chuma = 5.25mg

 • Magineziamu = 325mg

 • Manganaizi = 1.95mg

 • Sodiamu = 9mg

 • Zinki = 5mg

 • Fosifolasi = 660mg


Faida za alizeti


Alizeti huwa na faida zifuatazo;


 • Huchochea afya nzuri ya moyo kutokana na mafuta yake kutokuwa na kolestro mbaya ya LDL

 • Hupelekea afya nzuri ya ngozi kutokana na kuwa na wingi wa Vitamin A na E

 • Huchochea mwili kuwa na nguvu kutokana na kuw ana wanga

 • Huweza kuimarisha nywele na kuzifanya zisikatike katike kutokana na kuwa na vitamini E

 • Huimarisha kinga ya mwili kutokana na kuw na madini ya selenium na vitamini

 • Husaidia mfumo wa umeng’enyaji wa chakula kwenda kwa haraka

 • Husaidia kupunguza kolestro ya LDL mwilini

 • Husaidia kupunguza hatari ya kupata saratani kutokana na kuwa na kuwa na antioksidanti kwa wingi

 • Hupunguza inflamesheni mwilini, hivyo huwa na faida kwa wagonjwa watu wenye pumu

 • Husaidia kupunguza chunusi kwa kuwa na wingi wa Vitamin A na E

 • Husaidia kupunguza hali ya kuzeeka mapema kutokana na wingi wa antioksidanti

 • Hupunguza hatari ya kupata shinikizo la damu la juu

Imeboreshwa,
4 Desemba 2021 16:59:48
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

 1. Global Health Benefits of sunflower. https://globalhealing.com/natural-health/health-benefits-of-sunflower-seeds/amp/. Imechukuliwa 10/4/2020

 2. Good food for good. Sunflower Oil. https://goodfoodforgood.ca/2019/06/06/good-food-for-good-amazing-benefits-of-sunflower-seeds/. Imechukuliwa 10/4/2020

 3. EATING WELL SUNFLOWER OIL. http://www.eatingwell.com/article/2059940/sunflower-seeds-nutrition/. Imechukuliwa 10/4/2020

 4. Health Line Sunflower oil. https://www.healthline.com/nutrition/sunflower-seeds. Imechukuliwa 10/4/2020

 5. Seeds, sunflower seed kernels, dried. https://nutritiondata.self.com/facts/nut-and-seed-products/3076/2. Imechukuliwa 10/4/2020

 6. Manwaring, W H. “Nutritional Value of Sunflower Seed.” California and western medicine vol. 63,3 (1945): 112.

 7. Ciarka D, et al. (2009). "Allelopathic potential of sunflower. I. Effects of genotypes, organs and biomass partitioning". Allelopathy Journal. 23 (1): 95–109.

 8. Marzinek, et al. (September 2008). "Cypsela or achene? Refining terminology by considering anatomical and historical factors". Revista Brasileira de Botânica. 31 (3): 549–553.

 9. Leather GR (1987). "Weed control using allelopathic sunflowers and herbicide". Plant and Soil. 98: 17–23.

bottom of page