Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Mangwella S, MD
Dkt. Peter A, MD
Jumapili, 21 Novemba 2021
Madini chuma
Chuma ni madini muhimu katika uzalishaji wa chembe nyekundu za damu mwilini. Upungufu wa madini haya hupelekea upungufu wa damu kutokana na upungufu wa madini chuma unaoweza kutoka kwa wajawazito au watu wanaopata kiasi kidogo cha madini chuma kwenye chakula. Mwili unapokosa madini chuma ya kutosha, hushindwa kuzalisha chembe nyekundu na hivyo kupelekea upungufu wa damu mwilini na mtu huwa na afya isiyo njema. Hali hii ya kupungukiwa na chembechebe nyekundu za damu mwilini huitwa ufungufu wa damu wa madini chuma.
​
Watu wengi barani afrika hawapati kiwango cha kutosha cha madini chuma kutoka kwenye vyakula vinavyoliwa, pia kuna sababu zingine zinazoweza kupelekea upungufu huu wa madini chuma kama kupotea kutokana na kutokwa na damu bila wewe kujua. Hivyo ni vema kupata madini chuma ya ziada ili kukidhi mahitaji ya mwili. Daktari wako anaweza kutambua unaupungufu wa madini chuma na kukupa ushauri endapo unahitaji madini chuma ya ziada mbali na unayopaka kutoka kwenye chakula.
​
Dalili
Upungufu wa madini chuma unaweza kuleta dalili zifuatazo;
Uchovu usio wa kawaida
Kuishiwa pumzi
kupungua kwa ufanisi wa utendaji kazi
Kushindwa kujifunza dalasani kwa watoto na watu wazima
Pia upungufu wa madini chuma humpelekea mtu kupata maambukizi ya magonjwa kirahisi
Hali zinazoongeza mahitaji ya madini chuma
Hali ambazo zinaweza ku ziada pelekea ukahitaji madini chuma ya ziada ni;
Matatizo ya kutokwa na damu
Kuungua
Kusafishwa damu kwa figo bandia
Magonjwa ya matumbo
Magonjwa ya mfuko wa chakula
Kuondolewa kwa mfuko wa chakula mwilini
Matumizi ya dawa za kuongeza idadi ya chembe nyekundu za damu
Kwa vichanga ambao wanakunywa maziwa ya kopo yenye madini chuma kidogo, wanatakiwa kupata nyongeza ya madini chuma.
Nani aamue uongeze kiwango chamadini chuma unachotumia?
Nyongeza ya madini chuma inabidi itolewe na daktari wako na si wewe kufanya uamuzi huo.
​
Vyanzo vya madini chuma
Vyanzo vya madini chuma ni pamoja na;
Nyama nyekundu(huwa na madini chuma kwa wingi sana)
Nyama ya kuku, samaki pia huwa na madini chuma lakini sio kwa wingi kama nyama nyekundu
Vyakula vya nafaka,maharagwe na baadhi ya mboga za majani(kama mchuchicha) huwa na madini chuma lakini huwa hayafyonzwi vema na matumbo.
​
Vyakula vinavyoongeza ufyonzwaji wamadini chuma
​
Vyakula vinavyoongeza ufyonzaji wa madini chuma katika chakula unachokula au dawa za kunywa ni vile vyenye vitamin C kwa wingi kama;
Machungwa
Ndimu
Limao)
Vyakula vinavyopunguza ufyonzwaji wamadini chuma
Vyakula vifuatavyo hupunguza ufyonzwaji wa madini chuma tumboni kama vitatumika masaa machache kabla au baada ya kula vyakula vyenye madini chuma.
Mayai
Spinachi
vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi
Kahawa
Chai
Fomu ya madini chuma
​
Madini chuma hupatikana kwenye fomu mbalimbali kama vile;
Kidonge, cha kutafuna
Kidonge cha kumeza
​
Majina ya dawa zenye madini chuma
Madini chuma hupatikana kwenye dawa zenye majina mabalimbali kama;
Hemovit
FEFO/ferrous sulphate and folic acid
Iron
Imeboreshwa,
21 Novemba 2021 12:06:41
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Who. Anaemia in women and children. Https://www.who.int/data/gho/data/themes/toics/anaemia_in_women_and_children
Bruno f. Sunguya et al. High burden of anaemia among pregnant women in tanzania: a call to address its determinants.https://nutritionj.biomedicentral.com/articles/1.11/s12937-21-72-0. Imechukuliwa 20.11.2021
Iron - health professional fact sheet – nih office of dietary suplements https://ods.od.nih.gov/factsheets/iron- healthprofessional/. Imechukuliwa 20.11.2021
NCBI. How can I get enough iron?. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK279618/. Imechukuliwa 20.11.2021
NHS. Iron. https://www.nhs.uk/conditions/vitamins-and-minerals/iron/. Imechukuliwa 20.11.2021