top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Charles W, MD

Ijumaa, 22 Oktoba 2021

Maharagwe
Maharagwe

Zipo aina tofauti za maharagwe kama maharage ya soya na maharage ya kawaida

Faida za maharagwe


Maharage kwa ujumla ni chanzo kikubwa cha protini (soya huongoza) kutoka katika mimea, protini hii husaidia kujenga mwili.

Protini hii huweza kujenga mwili kama misuli, kusaidia kuziba/kupona kwa vidonda/majeraha ya mwili n.k

Maharage ya soya yamekuwa yakitumika kutengeneza uji wa lishe kwa ajiri ya watoto na watu wazima.

lishe hii huwa ina mchanganyiko wa maharage, karanga, ulezi ama mchele, na wengine huweka dagaa pia

Kwa kutumia mchanganyiko huu unapata mwili weye afya na akili safi.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Maharage


 • Mafuta

 • Madini

 • Sukari

 • Nyuzilishe

 • Protini

 • Vitamini

 • Kabohaidreti

 • Maji


Kemikali muhimu inayopatikana kwenye Maharage


Maharage yana kemikali muhimu iitwayo Phenolic Acid.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Maharage yenye gramu 100


 • Nishati = 334kcal

 • Mafuta = 1.1g

 • Maji = 11.75g

 • Kabohaidreti = 61g

 • Sukari = 2.1g

 • Nyuzilishe = 15g

 • Protini = 23g


Vitamini zinazopatikana kwenye Maharage yenye gramu 100


 • Vitamini B1 = 0.068mg

 • Vitamini B2 = 0.215mg

 • Vitamini B3 = 2.110mg

 • Viatmini B5 = 0.780mg

 • Vitamini B6 = 0.397mg

 • Vitamini B9 = 394mcg

 • Vitamini C =4.5mg

 • Vitamini E =0.21mg

 • Vitamini K = 5.6mg


Madini yanayopatikana kwenye Maharage yenye gramu 100


 • Kalishiamu = 83mg

 • Kopa = 0.7mg

 • Floraidi = 2.2mg

 • Madini Chuma = 6.69mg

 • Magineziamu = 138mg

 • Manganaizi = 1.111mg

 • Fosifolasi = 406mg

 • Potashiamu = 1359mg

 • Sodiamu = 12mg

 • Zinki = 2.79mg


Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Maharage


 • Hupunguza uzito usiotakiwa.

 • HKupunguza kiwango cha sukari mwilini.

 • Hupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kupooza.

 • Huongeza kinga ya mwili na kusaidia ukuaji.

 • Huimarisha utendaji kazi wa moyo na kuzuia ugonjwa wa shinikizo la juu la damu.

 • Huimarisha utendaji kazi wa Ini.

 • Huongeza hamu ya kula.

 • Husaidia kwenye mchakato wa utengenezwaji wa chembe chembe nyekundu za damu.

Imeboreshwa,
21 Machi 2022 20:16:27
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

 1. Polak, Rani et al. “Legumes: Health Benefits and Culinary Approaches to Increase Intake.” Clinical diabetes : a publication of the American Diabetes Association vol. 33,4 (2015): 198-205. doi:10.2337/diaclin.33.4.198

 2. Beans .https://www.nutritionvalue.org/Beans%2C_raw%2C_mature_seeds%2C_red%2C_kidney_nutritional_value.html. Imechukuliwa tarehe 20 January 2022.

 3. Ganesan K., Xu B. Polyphenol-Rich Dry Common Beans (Phaseolus vulgaris L.) and Their Health Benefits. Int. J. Mol. Sci. 2017;18:2331. doi: 10.3390/ijms18112331. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7915747/.  Imechukuliwa tarehe 20 January 2022.

 4. Rizkalla SW, Bellisle F, Slama G. Health benefits of low glycaemic index foods, such as pulses, in diabetic patients and healthy individuals. Br J Nutr. 2002 Dec;88 Suppl 3:S255-62. doi: 10.1079/BJN2002715. PMID: 12498625. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/12498625/. Imechukuliwa tarehe 20 January 2022.

bottom of page