top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Peter R, MD

Dkt. Mangwella S, MD

Jumatano, 3 Novemba 2021

Maji ya nazi
Maji ya nazi

Maji ya nazi ni kimiminika kinachopatikana ndani ya nazi, kimiminika hiki hutokea punde tu unapoivunja nazi amabyo bado haijjakomaa. Ikumbukwe kuwa tui la nazi na maji ya nazi ni vitu viwili tofauti. Tui hupatikana baada ya kukamua nazi iliyokomaa.kama ilivyo vimiminika vingine, pia maji ya nazi yana manufaa kiafya kwa mwanadamu. Mara nyingi hutumika kama sharubati (juisi).


Viinilishe vinavyopatikana kwenye maji ya nazi


 • Protini

 • Nyuzilishe

 • Sukari

 • Kabohaidreti

 • Sodiamu

 • Mafuta

 • Maji


Viinilishe vinavyopatikana kwenye kikombe kimoja cha maji ya nazi


 • Nishati (kalori) - 46kcal

 • Protini - 1.7gm

 • Nyuzilishe - 2.6gm

 • Sukari - 6.3gm

 • Kabohaidreti - 8.9gm

 • Sodiamu - 250gm

 • Mafuta - 0.4gm


Vitamini zinazopatikana kwenye kila kikombe kimoja cha maji ya nazi


 • Vitamini A - 0.00mg

 • Vitamini b1 - 0.072mg

 • Vitamini b2 - 0.137mg

 • Vitamini b3 - 0.192mg

 • Vitamini b5 - 0.103mg

 • Vitamini b6 - 0.077mg

 • Vitamini b7 - 7.20mg

 • Vitamini c - 5.8mg


Madini yanayopatikana kwenye kila kikombe kimoja cha maji ya nazi


 • Kalishiamu - 57.6mg

 • Kopa - 0.096mg

 • Chuma - 0.70mg

 • Magineziamu - 60mg

 • Zinki - 0.20mg

 • Sodiamu - 252mg

 • Seleniamu - 2.4mg

 • Fosifolasi - 48mg

 • Potashiamu - 600mg


Faida zipatikanazo baada ya kutumia maji ya nazi


 • Kuupa mwili nguvu

 • Kurudisha na kupunguza upotevu wa maji mwilini

 • Kurutubisha mwili

 • Kuongeza kinga ya mwili

 • Kurutubisha ngozi

 • Kurekebisha homoni

Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:02:11
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

 1. Barclay, Eliza (15 August 2011). "Coconut Water To The Rescue? Parsing The Medical Claims". NPR

 2. Vita Coco coconut water settles class action lawsuit". Lexology. Manatt Phelps & Phillips LLP. 27 May 2012.

 3. Rees, Richard; Barnett, Joe; Marks, Daniel; George, Marc (September 2012). "Coconut water-induced hyperkalaemia". British Journal of Hospital Medicine.

 4. Crawford, Elizabeth (29 October 2014). "Coconut products can never claim to be 'healthy' because of the saturated fats, says legal expert". foodnavigator-usa.com.

bottom of page