Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
Ijumaa, 17 Desemba 2021
Maziwa ya soya
Ni maarufu miongoni mwa maziwa yote yenye asili ya mimea na yamesheheni protini nyingi kuliko maziwa mengine. Matumizi ya maziwa ya soya yaliyoongezewa virutubisho yanapendekezwa zaidi.
Maziwa ya soya au vinywaji vinavyotokana na soya vina lishe bora kuliko maziwa mengine yote asili ya mimea. Soya huwa na protini nyingi na mafuta yake ni ya afya, kutokana na kuwa na asidi ya mafuta yenye omega-3.
Sifa
Mbali na sifa za kawaida za maziwa yote, maziwa ya soya;
Yana madini ya chuma mara 15 zaidi ya maziwa ya ng’ombe.
Yana kalisi [yaliofungashwa, hivyo huwa na kiwango sawa kama maziwa ya ng’ombe[kiasi cha gramu 120 katika kila mililita 100].
Kuna uzalishaji ya chapa ya soya isiyorekebishwa kimaumbile
Lishe bora na kinga ya saratani
Maziwa ya soya ni maziwa pekee ya mimea ambayo kiwango chake cha virutubishi kinalingana na maziwa ya ng’ombe yakiwa na faida nyingi za afya. Uwezo wake wa kuzuia saratani ya matiti na tezi dume inajulikana, hasa inapotumika tangu ujana.
Hayana homoni za wanyama ukilinganisha na maziwa ya ng’ombe wa kisasa yaliyo na estrojeni na homoni zingine.
Kinga dhidi ya saratani ya matiti na tezi dume na ugonjwa wa mifupa dhaifu (osteoporosisi)
Hayachochei mzio, pumu na uzalishaji wa kamasi, kama inavyotokea kwa utumiaji wa maziwa ya ng’ombe.
Ufafanuzi kuhusu estrojeni itokanayo na mimea
Ingawa uwepo wa estrogen kwenye mimea unaweza leta mkanganyiko, madhara ya estrojeni ya mimea hayako sawa na yale ya estrojeni asili ya wanyama.
Estrojeni ya soya haipelekei kupata saratani kama ilivyo estrojeni kutoka kwenye dawa za uzazi wa mpango au vyakula vya wanyama, kinyume chake hukinga dhidi yake. Tafiti nyingi za maabara na epidemiolojia juu ya binadamu zinathibitisha hili.
Isoflavone za soya na estrojeni zingine za mimea zinapatikana sana katika vyakula vya mimea. Mbegu zote zina viwango mbalimbali vya kemikali hizi, hasa mimea jamii ya kunde. Kama estrojeni za mimea zingekuwa na madhara,wale wanaotumia mbegu kwa wingi kama sehemu ya lishe ya afya wangekuwa na hatari kubwa ya kupatwa na saratani. Hata hivyo, kiuhalisia inaonesha kinyume chake kabisa.
Tafiti nyingi hasi kuhusu matumizi ya chakula cha soya zimefanyika kwa wanyama na hazitumiki kwa binadamu.
Estrojeni za kwenye soya na mbegu zingine hazifanyi wanaume waonekane kama wanawake au kupata saratani. Kwa upande mwingine, estrojeni halisi iliyoko kwenye maziwa ya ng’ombe huhusianishwa na saratani ya tezi dume .
Wanawake ambao wamewahi kuwa na saratani ya ziwa wanaweza kutumia soya na mazao yake kwa kiasi cha kawaida.
Imeboreshwa,
17 Desemba 2021 05:15:25
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Messina, et al. “Soy and Health Update: Evaluation of the Clinical and Epidemiologic Literature.” Nutrients vol. 8,12 754. 24 Nov. 2016, doi:10.3390/nu8120754.
Rizzo, et al. “Soy, Soy Foods and Their Role in Vegetarian Diets.” Nutrients vol. 10,1 43. 5 Jan. 2018, doi:10.3390/nu10010043.
Rizzo, Gianluca. “The Antioxidant Role of Soy and Soy Foods in Human Health.” Antioxidants (Basel, Switzerland) vol. 9,7 635. 18 Jul. 2020, doi:10.3390/antiox9070635