Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, CO
Dkt. Benjamil L, MD
Jumatano, 3 Novemba 2021
Nazi
Nazi ni zao litokanalo na mti wa mnazi, ni jamii ya karanga ya juu ya ardhi. Tunapata nazi baada ya kubangua kutoka kwenye ganda (kokwa) lake. Umahiri na uzuri wa Nazi katika afya ya binadamu umekua ukizingumzwa tangu karne na karne (Zamani hizo). Hivyo basi wataalamu wengi wa afya duniani kote wamekua wakithibitisha kuwa nazi inafaa kwa matumizi ya Binadamu. Pia nazi imekua ikitumika kwa matumizi mbalimbali kama vile maziwa ya nazi, Maji ya nazi, Tui la nazi.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye nazi
Vitamini
Nyuzilishe
Mafuta
Protini
Madini
Kabohaidreti
Viinilishe vinavyopatikana kwenye nazi yenye gramu 100
Nishati (Kalori) - 354kcal
Protini - 3.3gm
Nyuzilishe - 9gm
Mafuta - 33.4gm
Kabohaidreti - 15.23gm
Vitamini zinazopatikana kwenye nazi yenye gramu 100
Vitamini A - 0.10mg
Vitamini B - 0.020mg
Vitamini C - 3.3mg
Vitamini E - 0.24mg
Folalesi - 26ug
Niasini - 0.54mg
Madini yanayopatikana kwenye nazi yenye gramu 100
Kalishiamu - 14mg
Kopa - 0.435mg
Chuma - 2.43mg
Zinki - 1.10mg
Fosifolasi - 113mg
Magineziamu - 32mg
Manganizi - 1.5mg
Faida zitokanazo na ulaji wa nazi
Kujenga mwili
Kuupa mwili nguvu
Kuimarisha mishipa ya damu
Kuboresha afya ya ngozi na nywele
Kufanya mwili kuwa Imara kwa kupunguza spidi ya kuzeeka haraka
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:01:26
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Brouwers, Lucas (August 1, 2011). "Coconuts: not indigenous, but quite at home nevertheless". Scientific American. Lutz, Diana (June 24, 2011). "Deep history of coconuts decoded"
Nayar, N. Madhavan (2016). The Coconut: Phylogeny, Origins, and Spread. Academic Press. pp. 51–66. ISBN 9780128097793.
Thampan, P.K. (1981). Handbook on Coconut Palm. Oxford & IBH Publishing Co.