top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Peter R, CO

Dkt. Mangwella S, MD

Alhamisi, 4 Novemba 2021

Ngano
Ngano

Unga wa ngano ni unga unaotokana na zao la nafaka la ngano, ambalo ni maarufu kwa sababu sifa zake za kuwa na madini na virutubusho ya kutosha. Unga wa ngano unapatikana karibu sehemu nyingi duniani. Zao hili huwa na kazi nyingi kama vile kutengeneza keki, maandazi, chapati n.k.

Watu wenye mzio na gluten wanapaswa kuepuka ngano kwa kuwa huwa na gluten kwa wingi.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye unga wa ngano


 • Kabohaidreti

 • Madini

 • Vitamini

 • Protini

 • Nyuzilishe

 • Sukari


Viinilishe vinavyopatikana kwenye unga wa ngano kwa kila gramu 100


 • Nishati - 420k

 • Maji - 11%

 • Protini - 3.2mg

 • Sukari - 0.4gm

 • Nyuzilishe - 10.7gm

 • Mafuta - 2.5gm

 • Kabohaidreti - 72gm


Madini yanayopatikana kwenye unga wa ngao kwa kila gramu 100


 • Kalisiamu - 34mg

 • Chuma - 3.88mg

 • Magneziam - 138mg

 • Sodiamu - 5mg

 • Zinki - 2.93mg

 • Potasiamu - 405mg

 • Fosforasi - 346mg


Vitamini zinazopatikana kwenye unga wa ngano kwa kila gramu 100


 • Vitamini B1 - 0.447mg

 • Vitamini B2 - 0.215mg

 • Vitamini B3 - 6.365mg

 • Vitamini B5 - 1.008mg

 • Vitamini B6 - 0.341mg


Kemikali zipatikanazo kwenye ngano


 • Gluten

 • Phylate


Faida za afya zinatokanazo na matumizi ya unga wa ngano

Faida za kiafya za ngano ni;


 • Huupa mwili nguvu

 • Huukinga mwili na saratani za aina mbalimbali

 • Huimarisha na kujenga mwili

Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:00:35
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

 1. Fraser, J. R (1951). "National flour survey 1946–1950". Journal of the Science of Food and Agriculture. 2 (5): 193–198.

 2. Fraser, J. R (1951). "National flour survey 1946–1950". Journal of the Science of Food and Agriculture. 2 (5): 193–198.

 3. Commons Sitting: Food Supplies: National Flour". Hansard. House of Commons of the United Kingdom. 27 October 1943. Imechukuliwa  1 .11.2021

 4. Wang, et al. (2005-02-17). "Impact of the fungal protease produced by Fusarium culmorum on the protein quality and breadmaking properties of winter wheat". European Food Research and Technology. Springer Science and Business Media LLC.

 5. Kınacı, et al. (2004). "Quality and yield losses due to sunn pest (Hemiptera: Scutelleridae) in different wheat types in Turkey".

bottom of page