Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
17 Februari 2026, 04:18:08
Papai: Faida za Kiafya
Papai ni tunda limekuwa likitumiwa na binadamu kwa ajili ya matibabu ya magonjwa ya tumbo. Tunda hili lina virutubisho vya kutosha, hupatikana katika ukanda wa tropiki, na hupatikana katika umbo na sura tofauti. Watu wengi wamekuwa wakiweka tunda hili kama saladi ya matunda mbalimbali. Papai huwa na sukari kiasi na vitamin kwa wingi, pamoja na madini kali
Virutubishi vya papai
Maelezo yanayofuata hapa chini yanahusu viinirishi na madini yaliyo kwenye tunda la papai
​
Vitamin
​
Papai huwa na vitamin nyingi kuliko matunda mengine yale uliyowahi kula, vitamin zinazopatikana katika papai huwa pamoja na Vitamin B6, Thiamine, Riboflavin, Folati, na Niasini, Kwa kifupi papai huwa na vitamin B kwa wingi na hivyo huweza kuwa kama Vitamin B complex ambayo husaidia mwili wako katika kazi mbalimbali.
Tafadhali soma kuhusu vitamin hizo kwa kubonyeza vitamin hiyo. Papai pia huwa na vitamin C ambayo huwa na umuhimu kuweka seli za mwili afya njema, na husaidia ufyonzaji wa chakula kwenye mfumo wa tumbo.
Madini
​
Papai pia huwa na kiasi kizuri cha madini kama madini ya manganese, madini kali,na madini chuma. Madini kali huwa kwa kiasi cha kutosha mabacho unahitaji kwa siku.
​
Faida za papai
Hupunguza uzito- Kwa sababu papai huwa na sukari kidogo na pia huweza kushibisha, mtu anayetumia papai tu huweza kupunguza uzito ikiwa atatumia papai
Tunda zuri kwa ajili ya wagonjwa wa kisukari kwa sababu lina sukari kiasi
Husaidia macho kuona vema kwa sababu huwa na vitmini A kwa wingi
Huimarisha mmeng’enyo wa chakula
Hukinga dhidi ya magonjwa ya maungio ya mwili
Husaidia kupunguza maumivu ya hedhi
Hupunguza kuzeeka haraka
Hukinga mtu dhidi ya saratani
Imeandikwa;
22 Oktoba 2021, 12:17:45
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
V Coothankandaswamy, et al. The Alternative Medicine Pawpaw and Its Acetogenin. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2890309/. Imechukuliwa 22.10.2021
YR Kong, et al. Beneficial Role of Carica papaya Extracts and Phytochemicals. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC8066973/. Imechukuliwa 22.10.2021
