top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Peter R, C.O

Dkt. Benjamin L, M.D

Ijumaa, 28 Januari 2022

Tini
Tini

Tini ni matunda madogo yanayotokana na miti midogo ya maua kutoka kundi la Ficus carica na familia ya Moraceae. Tini inakua imesheheni virutubisho na vitamini kwa wingi kuwezesha ujenzi wa mwili, kurekebisha sukari n.k


Viinirishe vinavyopatikana kwenye Tini


 • Mafuta

 • Kabohaidreti

 • Nyuzilishe

 • Protini

 • Sukari

 • Madini

 • Vitamini


Kemikali muhimu inayopatikana kwenye Tini


Tunda la Tini lina kemikali muhimu inayoitwa Cyanidin


Viinirishe vinavyopatikana kwenye Tini


 • Nishati = 74kcl

 • Jumla ya mafuta = 0.1g

 • Sukari = 16g

 • Nyuzilishe = 2.4g

 • Protini = 0.3g

 • Kabohaidreti = 19mg

 • Maji = 79.11g


Madini yanayopatikana kwenye Tini Zenye Gramu 100


 • Chuma = 0.37mg

 • Kalisiamu = 35mg

 • Magneziam = 17mg

 • Fosifolasi = 14mg

 • Potasiamu = 232mg

 • Sodiamu = 1mg

 • Manganizi = 0.128mg

 • Zinki = 0.15mg


Vitamini zinazopatikana kwenye Tini zenye gramu 100


 • Vitamin A = 7mcg

 • Vitamini B1 = 0.06mg

 • Vitamini B2 = 0.05mg

 • Vitamini B3 = 0.4mg

 • Vitamini B5 = 0.5mg

 • Vitamini B6 =0.113mg

 • Vitamini B9 = 6mcg

 • Vitamini C = 2mg

 • Vitamini E = 0.11mg

 • Vitamini K = 4.7mcg


Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Tini

 • Huimarisha mfumo mzima wa mishipa ya damu, hivyo kuzuia shinikizo la juu la damu.

 • Huimarisha kinga ya mwili na kuzuia saratani za aina mbalimbali.

 • Huimarisha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.

 • Huimarisha utendaji kazi wa mfumo wa fahamu.

 • Huimarisha afya ya ngozi

 • Hutibu kikohozi

 • Hurekebisha kiwango cha sukari mwilini, hivyo ni sahihi kutumiwa na wagonjwa kisukari

 • Hutibu na kuzuia tatizo la kuharisha

 • Hutibu na kuzuia minyoo tumboni

Imeboreshwa,
28 Januari 2022 08:14:45
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

 1. Figs nutritional value. https://www.nutritionvalue.org/Figs%2C_raw_nutritional_value.html?size=100+g&utm_source=share-by-url. Imechukuliwa 27/12/2021

 2. Subash S, Essa MM, Braidy N, Al-Jabri A, Vaishnav R, Al-Adawi S, Al-Asmi A, Guillemin GJ. Consumption of fig fruits grown in Oman can improve memory, anxiety, and learning skills in a transgenic mice model of Alzheimer's disease. Nutr Neurosci. 2016 Dec;19(10):475-483. doi:10.1179/1476830514Y.0000000131. Epub 2016 Mar 2. PMID: 24938828. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/24938828/. Imechukuliwa 27.12. 2021.

 3. Solomon A, Golubowicz S, Yablowicz Z, et al. Antioxidant activities and anthocyanin content of fresh fruits of common fig (Ficus carica L.) Journal of Agricultural and Food Chemistry. 2006;54(20):7717–7723. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3789402/. Imechukuliwa 27.12.2021.

bottom of page