Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Peter A, MD
Jumatano, 10 Novemba 2021
Vitamin B3
Upungufu hupelekea kuonekana kwa dalili za michomo kwenye ngozi, kuharisha, ugonjwa wa kusahau na michomo kwenye matumbo.
Majina mengine
Vitamin B3 kwa jina jingine Niacin
​
Dalili za upungufu wa Vitamin B3
Upungufu hupelekea kuonekana kwa dalili na viashiria vifuatavyo;
Magonjwa ya michomo kinga ya ngozi
Kuharisha
Ugonjwa wa kusahau
Magonjwa kutokana na michomo kinga kwenye matumbo.
Madhara ya vitamin B3
Madhara Vitamin B3 kutoka kwenye chakula
Ukipata vitamin B3 kwa wingi kutoka kwenye chakula bado haujajulikana kama kuna sababisha madhara mwilini.
Madhara ya vitamin B3 kutoka kwenye dawa
Ukinywa vidonge na kuzidisha dozi huweza kusababisha;
Kutokwa na jasho kwenye
Kuwashwa
Kuharibika kwa utulivu wa tumbo
Kunywa miligramu 750 za vitamin B3 kila siku kwa miezi mitatu mfululizo huweza sababisha;
Uharibifu wa ini
Kuzidisha dozi ya vitamin B3 huweza kusababisha;
Kichefuchefu
Sumu kwenye ini
​
Vyanzo
Chanzo cha vitamin B3 ni nini?
Vyanzo vya vitamin B3 ni;
Uyoga
Karanga
Mchele wa brauni
Mahindi
Mboga za kijani
Viazi vitamu
Viazi mviringo
Kunde
Karoti
Kungu
Nyama ya kuku
Samaki
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 12:40:33
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
NHS. https://www.nhs.uk/conditions/vitamins-and-minerals/vitamin-b/. Imechukuliwa 14.07.2020
Vitamin B. better health channel. https://www.betterhealth.vic.gov.au/health/healthyliving/vitamin-b. Imechukuliwa 14.07.2020
David O. Kennedy. B Vitamins and the Brain: Mechanisms, Dose and Efficacy—A Revie. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4772032/. Imechukuliwa 08.04.2021
R. A. Peters. THE VITAMIN B COMPLEX. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2457859/. Imechukuliwa 08.04.2021
Neuroton. https://www.amoun.com/leap-portfolio-project/neuroton-ampoules-tablet/.Imechukuliwa 08.04.2021
Fiona O’Leary, et al. Vitamin B12 in health and diseses. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3257642/. Imechukuliwa 08.04.2021
Vitamin B9 nutrition facts. https://www.nutri-facts.org/en_US/nutrients/vitamins/b9.html. Imechukuliwa 08.04.2021
Vitamin b9(folic fcid)https://www.hsph.harvard.edu/nutritionsource/folic-acid/. Imechukuliwa 08.04.2021