Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
Jumatano, 10 Novemba 2021
Vitamin B5
Upungufu wa vitamin B5 hutokea kwa nadra sana na ikitokea mara nyingi huwa kwa mtu mwenye utapiamlo. Dalili za upungufu ni pamoja na hisia za miguu kuchomachoma, kuwaka moto au ganzi.
Majina mengine
Vitamin B5 kwa jina jingine Pantothetiki asid
​
Dalili
Dalili za upungufu wa vitamin B5 huwa pamoja na;
Hisia za ganzi miguuni
Hisia za miguu kuwaka moto
hisia za miguu kuungua
​
Kuzidisha dozi
Dalili za kuzidisha dozi ya vitamin B5 ni;
Kichefuchefu
Kiungulia
Kuharisha
Vyanzo
Vyanzo vya vitamin B5 ni;
Majani ya kunde
Mbegu za kunde
Parachichi
Ngano isiyokobolewa
Uyoga
Viazi vitamu
Mbegu za alizeti
Mboja za majani
Mayai
Samaki
Matunda madogodogo
Ini
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 12:40:02
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
NHS. https://www.nhs.uk/conditions/vitamins-and-minerals/vitamin-b/. Imechukuliwa 14.07.2020
Vitamin B. better health channel. https://www.betterhealth.vic.gov.au/health/healthyliving/vitamin-b. Imechukuliwa 14.07.2020
David O. Kennedy. B Vitamins and the Brain: Mechanisms, Dose and Efficacy—A Revie. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4772032/. Imechukuliwa 08.04.2021
R. A. Peters. THE VITAMIN B COMPLEX. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2457859/. Imechukuliwa 08.04.2021
Neuroton. https://www.amoun.com/leap-portfolio-project/neuroton-ampoules-tablet/.Imechukuliwa 08.04.2021
Fiona O’Leary, et al. Vitamin B12 in health and diseses. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3257642/. Imechukuliwa 08.04.2021
Vitamin B9 nutrition facts. https://www.nutri-facts.org/en_US/nutrients/vitamins/b9.html. Imechukuliwa 08.04.2021
Vitamin b9(folic fcid)https://www.hsph.harvard.edu/nutritionsource/folic-acid/. Imechukuliwa 08.04.2021