Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Peter A, MD
Jumatano, 10 Novemba 2021

Vitamin B6
Upungufu husababisha dalili mbalimbali kama vile huzuniko, kuchanika pembe za midomo, na ulimi magonjwa ya michomo kinga kwenye ulimi (inayoleta maumivu ya ulimi), tumbo na ngozi n.k
Majina mengine
Vitamin B6 kwa jina jingine pairidoksin
Dalili za upungufu
Dalili za upungufu wa vitamin B6 ni pamoja na;
Kuchanika kwenye pembe za midomo
kuchanika kwa ulimi
Magonjwa ya michomo kiga kwenye ulimi(inayoleta maumivu ya ulimi), tumbo, michomo na ngozi
Kupasuka kwa ngozi
Matatizo ya mfumo wa fahamu
Kukosa usingizi
Kuchanganyikiwa
Kukasilika haraka
Huzuniko
Kutotulia
Kupotea fahamu za misuli
Kushindwa kutembea
Upungufu wa damu
Madhara ya upungufu kwa kichanga
Kama mtoto atakosa vitamin B6 akiwa tumboni huweza kumsababisha apate mtindio wa ubongo atakapozaliwa na matatizo mengine ya damu.
Madhara ya kuzidisha vitamin B6
Kama ukitumia dozi kubwa ya vitamin B6 huweza kusababisha maumivu ya mwili yatokanayo na mishipa ya fahamu.
Vyanzo
Vyanzo vya vitamin B6 ni nini?
Vyanzo vikuu vya vitamin B6 ni;
Ngano isiyokobolewa
Mchele wa kahawia
Mbogamboga za kijani
Mbegu za alizeti
viazi
maharagwe
Ndizi
Spinachi
nyanya
Parachichi
Karanga
Samaki tuna, salmon na lima
Pilipili
Nyama ya kuku
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 12:38:31
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
NHS. https://www.nhs.uk/conditions/vitamins-and-minerals/vitamin-b/. Imechukuliwa 14.07.2020
Vitamin B. better health channel. https://www.betterhealth.vic.gov.au/health/healthyliving/vitamin-b. Imechukuliwa 14.07.2020
David O. Kennedy. B Vitamins and the Brain: Mechanisms, Dose and Efficacy—A Revie. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4772032/. Imechukuliwa 08.04.2021
R. A. Peters. THE VITAMIN B COMPLEX. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2457859/. Imechukuliwa 08.04.2021
Neuroton. https://www.amoun.com/leap-portfolio-project/neuroton-ampoules-tablet/.Imechukuliwa 08.04.2021
Fiona O’Leary, et al. Vitamin B12 in health and diseses. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3257642/. Imechukuliwa 08.04.2021
Vitamin B9 nutrition facts. https://www.nutri-facts.org/en_US/nutrients/vitamins/b9.html. Imechukuliwa 08.04.2021
Vitamin b9(folic fcid)https://www.hsph.harvard.edu/nutritionsource/folic-acid/. Imechukuliwa 08.04.2021