top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Peter R, Co

Jumapili, 27 Machi 2022

Zukini
Zukini

Zukini ni aina ya boga mwitu kutoka kundi la Cucurbita pepo, huvunwa ingali bado changa na kutumika kama chakula baada ya kuchemshwa/kupikwa au kuokwa. Zukini hupendwa kutumiwa na jamii nyingi hiyo ni kutokana na uwepo wa madini na vitamini kwa ajili ya ukuaji wa miili yetu.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Zukini


  • Mafuta

  • Madini

  • Sukari

  • Nyuzilishe

  • Protini

  • Vitamini

  • Kabohaidreti

  • Maji


Kemikali muhimu zinazopatikana kwenye Zukini


Zukini ina kemikali muhimu ziitwazo Zeaxanthin na Dehydroascorbic Acid


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Zukini lenye gramu 100


  • Nishati = 34kcal

  • Mafuta = 0.3g

  • Maji = 88.11g

  • Kabohaidreti = 7.4g

  • Sukari = 9.6g

  • Nyuzilishe = 0.8g

  • Protini = 1g


Vitamini zinazopatikana kwenye Zukini lenye gramu 100


  • Vitamini A = 8mcg

  • Vitamini B1 = 0.034mg

  • Vitamini B2 = 0.075mg

  • Vitamini B3 = 0.355mg

  • Viatmini B6 = 0.122mg

  • Vitamini B9 = 17mcg

  • Vitamini C =12.6mg

  • Vitamini E =0.10mg

  • Vitamini K = 3.6mg


Madini yanayopatikana kwenye Zukini lenye gramu 100


  • Kalishiamu = 15mg

  • Kopa = 0.04mg

  • Madini Chuma = 0.31mg

  • Magineziamu = 15mg

  • Fosifolasi = 32mg

  • Potashiamu = 217mg

  • Sodiamu = 951mg

  • Zinki = 0.27mg


Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Zukini


  • Kuimarisha afya macho na kuongeza uwezo kuona na kupunguza magonjwa ya macho yatokanayo na uzee.

  • Kuimarisha kinga ya mwili

  • Kupunguza athari ya kupatwa na kansa ya tezi dume na kansa nyingine

  • Kuimarisha mfumo wa mmeng`enyo wa chakula

  • Kusaidia kupunguza uzito usiohitajika mwilini

  • Kushusha kiwango cha sukari mwilini

  • Kusaidia kuimarisha na kuboresha afya ya moyo

  • Kusaidia kuzuia kupatwa na ugonjwa wa rovu

Imeboreshwa,
27 Machi 2022 17:47:34
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

  1. Zucchini. https://www.nutritionvalue.org/Zucchini%2C_pickled_75535000_nutritional_value.html?size=100+g. Imechukuliwa tarehe 4 February 2022.

  2. Wang X, Tanaka M, Peixoto HS, Wink M. Cucurbitacins: elucidation of their interactions with the cytoskeleton. PeerJ. 2017 May 30;5:e3357. doi: 10.7717/peerj.3357. PMID: 28584704; PMCID: PMC5452965. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/28584704/. Imechukuliwa tarehe 4 February 2022.

  3. Cha KH, Koo SY, Lee DU. Antiproliferative effects of carotenoids extracted from Chlorella ellipsoidea and Chlorella vulgaris on human colon cancer cells. J Agric Food Chem. 2008 Nov 26;56(22):10521-6. doi: 10.1021/jf802111x. PMID: 18942838. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/18942838/. Imechukuliwa tarehe 4 February 2022.

  4. Role of Zucchini and Its Distinctive Components in the Modulation of Degenerative Processes: Genotoxicity, Anti-Genotoxicity, Cytotoxicity and Apoptotic Effects. Written by Damián Martínez-Valdivieso, Rafael Font et al. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5537869/. Imechukuliwa tarehe 4 February 2022.

bottom of page