Kamusi Tiba ya ULY CLINIC
Benign positional vertigo
Ni neno tiba lenye jina la kiswahili la "Kizunguzungu cha mkao kisicho hatari"
ambapo ni hali ya mfumo wa usawa wa mwili inayotokea pale chembe ndogo za kalsiamu zinapohama kutoka sehemu yake ya kawaida na kuingia ndani ya mfereji ya nusu duara ya sikio la ndani na kusababisha upotoshaji wa taarifa za mkao wa kichwa zinazopelekwa kwenye ubongo, hali inayozalisha hisia ya mzunguko kila mtu anapogeuza au kuinamisha kichwa.

Benign tumor
Ni neno tiba lenye jina jingine la "Uvimbe usio saratani" ambao ni ukuaji usio wa kawaida wa seli unaounda uvimbe lakini hauonyeshi tabia za uvimbe was aratani. Seli zake hukua polepole, hubaki katika eneo lake la asili, na hazisambai kwenda sehemu nyingine za mwili. Kwa kawaida huwa na mipaka iliyo wazi na mara nyingi husukuma na kubana tishu jirani badala ya kuzivamia. Ingawa si hatari kama saratani, unaweza kusababisha matatizo kulingana na ukubwa na mahali ulipo.
Blast lung injury
Ni neno tiba lenye jina la kiswahili la "Jeraha la Pafu la Mlipuko" ambapo ni aina ya jeraha la ndani linalotokea pale mawimbi ya shinikizo kutoka kwenye mlipuko yanapopitia kwenye kifua na kuathiri mapafu. Ni moja ya majeraha hatari yanayoweza kutokea katika matukio ya milipuko, hata bila kuonekana kwa jeraha la nje kwenye kifua.

