top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Kipimo cha kuotesha usaha ni nini?

Kipimo cha kuotesha usaha

Pia huitwa kipimo cha kuotesha vimelea kwenye usaha, ni kipimo cha maabara kinachotumika kubaini bakteria au vimelea wengine wanaosababisha maambukizi kwenye kidonda, jipu au sehemu yenye usaha. Sampuli ya usaha huchukuliwa kutoka kwenye eneo lililoathirika na kupelekwa maabara kwa ajili ya kuotesha na kutambua kimelea kinachosababisha maambukizi.

Kipimo cha usikivu wa bakteria kwenye dawa

Kipimo cha usikivu wa fangasi kwenye dawa ni nini?

Kipimo cha usikivu wa fangasi kwenye dawa

Pia huitwa kipimo cha kuotesha fangasi na kuangalia usikivu wao kwenye dawa, ni kipimo cha maabara kinachotumika kutambua fangasi wanaosababisha maambukizi na kubaini dawa za kuua fangasi ambazo fangasi hao ni sikivu au sugu nazo. Sampuli inaweza kuchukuliwa kutoka kwenye ngozi, kucha, nywele, usaha, majimaji ya mwili au sehemu nyingine kulingana na eneo la maambukizi.

Kipimo cha usikivu wa virusi kwenye dawa ni nini?

Kipimo cha usikivu wa virusi kwenye dawa

Pia huitwa kipimo cha kuotesha virusi na kuangalia usikivu wao kwenye dawa, ni kipimo cha maabara kinachotumika kutambua virusi katika sampuli ya mgonjwa na kutathmini mwitikio wa virusi hao kwa dawa za kudhibiti virusi. Tofauti na bakteria, virusi havioti kwenye mazingira ya kawaida ya maabara, hivyo hutumia seli hai maalum kwa ajili ya kuvitambua na kuvichunguza.

Kirusini

Kirusini

Ni neno la kitiba linalomaanisha kimelea jamii ya kirusi kinachosababisha homa ya kirusini, virusi hivyo ni kirusini A, B, C, D na kirusini E

bottom of page