top of page

Kamusi Tiba ya ULY CLINIC

Anafailaksis ni nini?

Anafailaksis

Anafailaksis ni mzio mkali na wa haraka unaoweza kutokea dakika chache baada ya mtu kutumia dawa, kula chakula, au kugusana na kitu kinachosababisha mzio kwake. Ni hali hatari ambayo huhitaji huduma ya haraka ya kitabibu kwa sababu inaweza kuathiri kupumua na mzunguko wa damu.

Anajizia ni nini?

Anajizia

Ni upotevu wa hisia kwenye maumivu, ni ishara muhimu ya ugonjwa katika mfumo wa kati wa fahamu, na mara nyingi hutoa ishara ya sehemu gani haswa ya uti wa mgongo ina shida.

Analgesia ni nini?

Analgesia

Ni hali ya kupunguzwa au kuondolewa kwa maumivu bila kupoteza hisia za kugusa au hisia nyingine mwilini. Hii hutokea kwa kutumia dawa au mbinu nyingine za kutuliza maumivu.

Anaphylaxis ni nini?

Anaphylaxis

Ni mwitikio mkali wa kinga mwilini unaotokea ghafla baada ya mtu kuathirika na mzio, na unaweza kusababisha dalili za kupumua kwa shida, kushuka kwa shinikizo la damu, na hata kifo ikiwa hatatibiwa haraka.

Anisocoria ni nini kwa kiswahili?

Anisocoria

Ni hali ambapo wanao wana ukubwa tofauti wa mduara wa pupu (pupil) wa macho yao, hali inayoweza kuwa ya kawaida au ishara ya ugonjwa wa mfumo wa neva.

bottom of page