top of page
Kamusi Tiba ya ULY CLINIC
Ugonjwa wa Crohn
Ni ugonjwa wa muda mrefu unaosababisha uchochezikinga kwenye sehemu mbalimbali za mfumo wa chakula, kuanzia mdomoni hadi kwenye njia ya haja kubwa. Mara nyingi huathiri sehemu ya mwisho ya utumbo mdogo na mwanzo wa utumbo mpana, lakini unaweza kutokea katika sehemu nyingine za mfumo wa chakula.
Ugonjwa wa seliaki
Ni ugonjwa wa mfumo wa kinga ya mwili ambapo ulaji wa gluteni husababisha mfumo wa kinga kushambulia utando wa ndani wa utumbo mdogo. Gluteni hupatikana hasa kwenye nafaka kama ngano, shayiri na rai. Hali hii inaweza kuharibu vinyweleo vidogo vya utumbo vinavyosaidia kufyonza virutubisho kutoka kwenye chakula.
bottom of page


