USHAURI WA MATUMIZI YA DAWA KIPINDI CHA UJAUZITO NA KUNYONYESHA

Efavirenz na ujauzito
Taarifa za binadamu zipo chache sana kuruhusu kutabiri kuhusu hatari kwa kijusi tumboni na madhaifu ya kiuumbaji itakapotumika wakati wa ujauzito. Madhara ya kiuumbaji yaliyoonekana kwa nyani na panya inatoa ushuhuda kuwa na uwezekano mkubwa wa hatari kwa binadamu. Dawa hii huweza kupita kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na hivyo kuongezeka kwa hatari ya mtoto. Ripoti ya nyani ilionyesha kutokea kwa mgongo wazi (myelomeningocele) kutokana na matumizi ya dawa hii. Kwa ujumla wake, taarifa bado hazitoi majibu moja kwa moja kwamba efavirenz ni sumu kwa kichanga wa binadamu na hivyo isisitishwe kwa endapo ni muhimu kutumika kwa mama mjamzito.

Rifampin na ujauzito
Tafiti nyingi zimechunguza matibabu ya Kifua kikuu kwa kutumia dawa hii na zote zilihitimisha kuwa rifampin haikuwa na uwezo wa kusababisha madhaifu ya kimaumbile kwa kijusi tumboni na hivyo kupendekeza dawa hii na isoniazid kutumika katika matibabu ya TB. Tafiti zingine zingine pia zimeonyesha kutokuwepo kwa madhara kwa kichanga.Endapo itatumika kwa watoto, inashauriwa kutumia dawa hii pamoja na vitamin K ili kumkinga kichanga kuumwa ugonjwa kuvuja damu wenye jina la hemorrhagic disease of the newborn.

Didanosine na ujauzito
Kuna ripoti za ongezeko la hatari endapo la madhaifu ya kuzaliwa kwa kichanga endapo itatumika baada ya kipindi cha kwanza cha ujauzito, hata hivyo hatari ya kupata tatizo imepungua licha ya ongezeko la watumiaji. Theori zinasema kwamba endapo itatumika wakati wa kuchavushwa kwa yai, itafanya mimba isitungishwe kwa kuwa huwa sumu kijusi kwa wanyama, hii haijafanyiwa uchunguzi kwa binadamu. Hivyo endapo dawa hii iatapenekezwa kutumika, isisitishwe kwa sababu ya ujauzito.

Adefovir na ujauzito
Ni dawa ya kutibu maambukizi ya virusi ilio ambayo inafanana na adenosine monophosphate.Taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo kwa hatari kidogo,licha ya taarifa za binadamu kuwa chache. Endapo itapendekezwa kutumika kwenye matibabu, inatakiwa isisitishwe kutumika kwa sababu ya ujauzito.

Rifapentine na ujauzito
Rifapentine ilikuwa sumu na kuhusiana kusababisha madhaifu ya kiuumbaji kwa kijusi ilipotumika kwenye majaribio mawili ya wanyama wajawazito kwa kutumia dozi inayokaribia kufanana na ile ya binadamu.. uzoefu kwa binadamu ni kutoka kwa wajawazito watatu, wajawazito wawili waliotumia waliishia mimba kutoka kwenye kipindi cha kwanza cha ujauzito. Ingawa wajawazito hawa walikuwa na vihatarishi vingine vilivyoweza kusababisha pia mimba kutoka, madhara yaliyojitokeza yanatosha kuashiria kutumika kwa umakini dawa hii inapotumiwa wakati ujauzito mdogo. Mpaka pale taarifa zingine zitakapokuwepo kupinga hii, matumizi ya rifapentine yanatakiwa kuepukwa kwneye kipindi cha kwanza cha ujauzito.

Rifabutin na ujauzito
Hakuna taariza inayoelezea matumizi ya rifabutin kwa binadamu wajawazito, taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo na hatari kidogo ya kupata madhaifu ya kiuumbaji wa watoto wanaozaliwa na wanyama wajawazito waliotumia dawa hii. Hata hivyo, licha ya hatari hiyo kwa wanyama, faida za matumizi kwa binadamu ni kubwa kuliko madhara yanayoweza kujitokeza. Inapoanzishwa haitakiwi kuacha tumika kwa sababu ya ujauzito.

Pyrazinamide na ujauzito
Ni dawa mojawapo inayotumika kwenye matibabu ya kutibu Kifua kikuu (TB) iliyotokana na niacinamide. Hakuna taari za matumizi kwa wanyama wajawazito zinazoendana na dawa hii n ahata hivyo taarifa za matumizi kwa binadamu wajawazito zinaonyesha kutokuwepo na hatari ya kupata madhaifu ya kiuumbaji kwa watoto wanaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii. Hivyo kutokana na TB kuwa hatari zaidi kuliko madhara ya dawa hii, inashauriwa endapo imeanzishwa, isisitishwe kwa sababu ya ujauzito.

Isoniazid na ujauzito
Isoniazid haionekani kuwa kundi la dawa zinazofahamika kusababisha madhaifu ya kiuumbaji kwa watoto wanaozaliwa na wamama waliotumia dawa hii wakati wa ujauzito. Inashauriwa kuendelea kutumia dawa hii endapo imechaguliwa kutumika kwa sababu hatari za TB kwa mama ni kubwa kuliko madhara yanayoweza kujitokeza kwa mtoto kutokana na kutumia dawa hii.

Ethionamide na ujauzito
Ingawa tafiti za wanyama zinaonyesha kuwepo na hatari ya kutokea madhaifu ya kimaumbile kwa watoto wanaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii , taarifa za binadamu zinapendekeza kuwa hatari iliyopo ni kidogo na endapo imependekezwa tumika, isisitishwe kutumika kwa sababu ya ujauzito.

Trimethoprim na ujauzito
Trimethoprim inayofahamika kusababisha madhaifu ya kiuumbaji kwa vichanga kwa binadamu na wanyama. Madhaifu ya kiuumbaji kwa vichanga wanaozaliwa ambayo yamekuwa yakihusiana na matumizi ya dawa hii kwa wamama wajawazito ni pamoja na madhaofu ya moyo na mfumo wa fahamu pamoja na mdomo sungura. Matumizi ya Folic acid kiasi cha miligramu 0.4 kwa siku unatakiwa kufanyika kabla ya kushika mimba ili kuzuia kutokea kwa madhaifu hayo.


