top of page

USHAURI WA MATUMIZI YA DAWA KIPINDI CHA  UJAUZITO NA KUNYONYESHA

Vancomycin na ujauzito

Vancomycin na ujauzito

Vancomycin ni dawa ya antibayotiki inayotumika kutibu bakteria wa gram-positive. Dawa hii haijaonekana kusababisha madhaifu ya kimaumbile kwa vichanga wanaozaliwa na wamama waliotumia dawa hii.

Tinidazole na ujauzito

Tinidazole na ujauzito

Taarifa za uzoefu wa matumizi ya tinidazole kwa binadamu wajawazito zipo chache sana. Hata hivyo kunaonekana kuwepo kwa ongezeko kiasi la vifo vya watoto kwenye ujauzito wa wanyama walipotumia inayokaribiana na ile ya binadamu. Hakuna ushahidi mwingine unaosema kutokea kwa madhaifu ya kiuumbaji kwa vichanga waliozaliwa na wanyama waliotumia dawa hii. Tinidazole hufanana kikemia na dawa ya metronidazole. Itakuwa si hekima hata hivyo kufanya mbadala kutibu magonjwa yanayotibiwa na metronidazole kwa kutumia dawa hii. Tinidazole inatakiwa kutumika pale tu endapo metronidazole imefeli kufanya kazi ya kuondoa maradhi. Hata hivyo ni mpaka pale taarifa zaidi zitakapopatikana, ni vema kuzuia kutumia tinidazole katika kipindi cha kwanza cha ujauzito.

Ampicillin na ujauzito

Ampicillin na ujauzito

Dawa jamii ya penicillin huchukuliwa kama dawa zenye hatari kidogo kipindi chochote kile katika ujauzito. Uchunguzi huu unawezekana kuwa haujarekebishwa kwa dawa jamii ya aminopenicillins kama ampicillin na Amoxicillin kwa sababu kuna ushahidi kuwa kutumia dawa hizi kipindic ha kwanza cha ujauzito huongeza hatari ya madhaifu ya kiuumbaji kwa watoto wanaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii kama mdomo sungura. Hata hivyo kihatarishi huwa ni kidogo na mahusiano haya yanatakiwa kufanyiwa uchunguzi.

Amphotericin B na ujauzito

Amphotericin B na ujauzito

Ingawa tafiti za wanyama zinaonyesha kuwa na hatari ya kusababisha madhaifu ya kimaumbile, hakuna maudhi mabaya yaliyowahi kuripotiwa kutokea kwa kijusi na vichanga waliozaliwa na mama aliyetumia dawa hii kwnye ujauzito. Dawa hii hupita kwenye kondo na kuingia kwa mtoto na kiwango kwa mtoto hufikia kile kwenye damu ya mama.

Flucytosine na ujauzito

Flucytosine na ujauzito

Flucytosine huvunjwa mwilini kuwa kemikali ya 5-fluorouracil, kemikali inayofahamika kuwa teratogen(husababisha madhaifu ya kiuumbaji kwa mtoto) hivyo endapo inawezekana, usitumie kwenye kipindi cha kwanza cha ujauzito

Fluconazole na ujauzito

Fluconazole na ujauzito

Ingawa taarifa zipo chache, matumizi ya fluconazole kipindi cha kwanza cha ujauzito huonekana kuongeza hatari ya kuzaa watoto wenye madhaifu ya kiuumbaji endapo dozi endelevu ya gramu 400 kwa siku au au zaidi itatumika. Madhaifu ya kiuumbaji hufanana nay ale ya Antley-Bixler syndrome. Mwandishi anaelezea kuwa dozi ndogo huwa haina madhara, kama ile inayotumika kutibu fangasi ukeni. Endapo dawa hii ni lazima kutumika katika matibabu ya maambukizi ya fangasi katika kipindi cha kwanza cha ujauzito, mama mjamzito anatakiwa kuelezwa kuhusu hatari ya kupata mtoto mwenye madhaifu ya kiuumbaji.

Ketoconazole na ujauzito

Ketoconazole na ujauzito

Ketoconazole ni yenye uwanja mkubwa wa kutibu fangasi aina mbalimbali, dawa hii imekuwa ikitumika bila kuleta mdhara kwa kichanga kwenye matibabu ya fangasi ukeni kwa mama mama mjamzito.Dawa hii ipo kundi sawa na watoto wa imidazole kama butoconazole, clotrimazole, econazole, miconazole,oxiconazole, sertaconazole,sulconazole, na tioconazole.

Itraconazole na ujauzito

Itraconazole na ujauzito

Itraconazole ni dawa ya kutibu fangasi jamii ya triazole. Uzoefu wa matumizi ya dawa hii kwenye ujauzito unaonyesha kuwepo kwa hatari kidogo sana ya madhaifu ya kiuumbaji kwa vichanga wanaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii wakati wa ujauzito. Hata hivyo dawa zingine za triazole fluconazole, imeonyesha mahusiano kusababisha madhaifu ya kimaumbile kwa mtoto, mahusiano hayo yanahisiwa kuhusiana na dozi iliyotumika. Kwa dawa ya itraconazole, taarifa za wanyama haziwezi kujitosheleza kutafsiri kuwa sumu kwa binadamu mjamzito. Hivyo ni vema dawa hii ikazuiwa kipindi cha kwanza cha ujauzito kama ikiwezekana. Endapo matumizi ya dawa hii ni lazima kwenye kipindi cha kwanza cha ujauzito, mama anatakiwa ashauriwe kuwa hatari ya madhaifu kwa kichanga ni ndogo san ahata kama yapo.

Ectasy  na ujauzito

Ectasy na ujauzito

Ectasy ipo kundi moja na dawa jamii ya amphetamine, hufanya kazi kwa kusisimua mfumo wa kati wa fahamu na kufanya mtu ajihisi mtulivu na mwenye furaha.

Butoconazole na ujauzito

Butoconazole na ujauzito

Butoconazole hupatikana kama krimu ya kupaka kwa wajawazito wenye tatizo la fangasi. Taarifa chache kutoka kwenye binadamu wajawazito zinaweka dawa hii kwenye kundi la hatari kiasi cha madhaifu kwa mtoto.

Clotrimazole na ujauzito

Clotrimazole na ujauzito

Ufyonzwaji wa clotrimazole ni mdogo sana kwa mtu anayeweka kidonge ukeni au kupaka kwneye ngozi. Tafiti tatu kubwa zilizofanyika zimeonyesha kuwa, hakuna uhusiano wa matumizi ya dawa hii na kusababisha magonjwa ya madhaifu ya kiuumbaji kwa vichanga wanaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii.

Hata hivyo tafiti moja imeonyesha uhusiano mkubwa wa ongezeko la mimba kutoka kwa watumiaji wa dawa hii kutibu fangasi ukeni kwenye kipindi cha kwanza cha ujauzito.

Kutokana na tafiti hii, ni vema kuepuka kutibu ugonjwa wafangasi ukeni au kupaka sehemu kubwa ya mwili dawa hii mpaka pale kutakapokuwa na taarifa nyingi zaidi zinazoweza thibitisha mahusiano haya.

Econazole na ujauzito

Econazole na ujauzito

Matumizi ya dawa ya kupaka ya econazole hayaonekaini kusababisha hatari ya madhaifu kwa mtoto anayezaliwa na mama aliyetumia dawa hii kwenye ujauzito.Hakuna hatari iliyoonekana pia ya kusababisha madhaifu ya kiuumbaji kwa watoto wa wanyama wajawazito waliopewa dawa hii kwa njia ya kunywa na kuchoma kwenye ngozi, njia zinazoongeza kwa kiasi kikubwa kiini cha dawa kwenye damu, na kufanya dozi kuwa kubwa zaidi ya ile inayokuwa sumu kwa wanyama lakini ni salama kwa binadamu.

Matumizi ya dawa hii kupata huwa yana hatari kiasi au kutokuwepo kabisa. Hata hivyo tafiti moja imeonyesha uhusiano mkubwa wa ongezeko la mimba kutoka kwa watumiaji wa dawa hii kutibu fangasi ukeni kwenye kipindi cha kwanza cha ujauzito.

Hata hivyo tafiti moja imeonyesha uhusiano mkubwa wa ongezeko la mimba kutoka kwa watumiaji wa dawa hii kutibu fangasi ukeni kwenye kipindi cha kwanza cha ujauzito. Kutokana na tafiti hii, ni vema kuepuka kutibu ugonjwa wafangasi ukeni au kupaka sehemu kubwa ya mwili dawa hii mpaka pale kutakapokuwa na taarifa nyingi zaidi zinazoweza thibitisha mahusiano haya.

bottom of page