USHAURI WA MATUMIZI YA DAWA KIPINDI CHA UJAUZITO NA KUNYONYESHA

Erythromycin na ujauzito
Ripoti nyingi za dawa hii, ikihusisha tafiti moja iliyofanyika kwa wanyama hazijaonyesha ushahidi wa madhara ya uumbaji kwa kichanga endapo itatumika. Ingawa ripoti zinaonyesha kuhusiana na madhaifu ya uumbaji wa moyo, mchunguzaji hakuweza onyesha ushahidi thabiti kama kweli madhara hayo yanatokana na dawa hii. Kwa sababu tafiti nyingi hazionyeshi madhara ya kwenye ujauzito na kichang, dawa hii inaweza kutumika kipindi cha ujauzito endapo itatakiwa tumika.

Amoxicillin na ujauzito
Dawa jamii ya penicillins are huchukuliwa kama dawa zenye hatari kidogo kuleta matatizo kwenye ujauzito. Mapitio ya hatari yanawezekana hayajafanyiwa maboresho kwenye dawa aina mbili jamii ya aminopenicillin yaani ampicillin na amoxicillin kwa sababu ya kuwepo kwa ushahidi wa kutosha.

Ivermectin na ujauzito
Ivermectin ilikuwa kisababishi cha ulemavu kwa kichanga kwenye tafiti za wanyama jamii tatu, lakini kwenye dozi ambayo ni sumu kwa binadamu. Hakuna taarifa za kusababisha matatizo ya kiuumbaji kwa kichanga zilizoonekana kwenye taarifa chache za matumizi wakati wa ujauzito. Mapitio ya shirika la afya duani ya mwaka 1997 kuhusu taarifa za dawa hii yalitoa uamuzi kwamba, kutokana na hatari kubwa ya mama kupata upofu wa mtoni (usubi) kutoka kwenye maambukizi ya onchocerciasis, na kukosekana kwa taarifa za maudhi kwenye ujauzito, matumizi ya ivermectin kipindi cha kwanza cha ujauzito, yanaweza kukubalika.
Praziquantel na ujauzito
Praziquantel si dawa inayosababisha matatizo ya kiuumbaji kwa kichanga, hata hivyo taarifa za matumizi kwa binadamu ni chache. Kutokuwepo kwa taarifa inafanya kutoweza jua madhara yaliyopo kwa watumiaji wa dawa hii. Taarifa za mpya zinaonyesha kuwa dawa hii inaweza kusababisha saratani au kubadilisha vina saba vinasaba vya binadamu haswa kwenye nchi ambazo dawa hii inatumika sana au kuna maambukizi makubwa ya mnyoo 'Trematodes' na 'Cestodes'

Mebendazole na ujauzito
Mebendazole inatumika kipindi cha ujauzito kwenye matibabu ya minyoo jamii ya 'Ascaris lumbricoides' kwa jina jingine ' Roundworm', 'Trichuris trichiura' au 'Whipworm' na 'Enterobius vermicularis' kwa jina jingine 'Threadworm', 'Seatworm' au , 'Pinworm'. Dawa piperazine inaweza kutumiaka pia kwa matibabu ya minyoo hii kama kutokana na mapendekezo ya tafiti zingine.

Paracetamol na ujauzito
Acetaminophen(parasetamol au panado) imekuwa ikitumika mara nyingi katika kipindi chochote katika ujauzito. Ingawa ilifahamika kutokuwa na hatari kwa kichanga, kuna baadhi ya ripoti zimehoji kuhusu hili haswa kwa wamama wanaotumia dawa hii kwa muda mrefu au kwa wamama wenye jeni tofauti. Taarifa zaidi zinahitajika kupatikana ili kuthibitisha endapo kweli hakuna madhara yoyote kwa kijusi, hata hivyo inashauriwa isitumike mara kwa mara kipindi cha ujauzito.
Acamprosate na ujauzito
Kwenye tafiti zilizoanyikwa kwa panya, inayonyesha kuwa acamprosate ilikuwa sumu kweney uumbaji wa kijusi kwenye dozi ya kawaida anayoweza kutumia binadamu. Matatizo yaliyokuwa yanatokea kwa panya ni pamoja na kutofanyika vema kwa Iris, kuzaliwa na madhaifu ya macho na madhaifu kuhama sehemu yake asili mshipa wa damu wa subclavian artery. Hakuna tafiti zilizofanyika kwa binadamu kwa kuwa dawa hii ni sumu kwa binadamu.



