Sehemu hii utasoma kuhusu hali na magonjwa mbalimbali
Phecomelia
Ulemavu unaotokana na kutofanyika kikamilifu au kukosekana kabisa kwa miguu na mikono kunakochangiwa sana na matumizi ya dawa ya ukoma yenye jina la thalidomide wakati wa ujauzito.
Virusi vya corona ni familia kubwa ya virusi inayosababisha binadamu kuugua, mtu anaweza kupata dalili kali na kutokwa mafua au kuwa na dalili kali na za ghafla zaidi kwenye mfumo wa upumuaji.
Wasiwasi kwa watu wengi huja na kuondoka, kama wasiwasi unadumu, hupunguza thamani ya maisha ya mtu na hivyo huishi bila kujiamini na kushindwa kushiriki vema kwenye kazi.
Uteja ni hali ya mwili kutegemea dawa zisizoruhusiwa au yale yanayoruhusiwa kisheria ambayo huleta hali ya kuufurahisha mwili lakinimwisho wake hupelekea mwili kushindwa kuishi pasipo matumizi ya dawa hizo.