top of page

Magonjwa na saratani mbalimbali

Sehemu hii utasoma kuhusu hali na magonjwa mbalimbali

Fangasi kwenye damu (candidaemia)

Fangasi kwenye damu (candidaemia)

Fangasi kwenye damu (candidaemia) ni maambukizi hatari ya fangasi jamii ya Candida ndani ya damu, yanayowapata zaidi wagonjwa waliolazwa muda mrefu, wenye mipira ya mishipani, wanaotumia antibiotiki nyingi, watoto njiti na wenye kinga dhaifu. Huleta homa isiyopona kwa antibiotiki na sepsisi. Hutibiwa hospitalini kwa dawa za fangasi za mshipani.

Kifafa kwa watu wazima (epilepsy)

Kifafa kwa watu wazima (epilepsy)

Kifafa (epilepsy) ni ugonjwa wa ubongo unaosababisha degedege zinazojirudia kutokana na shughuli za umeme zisizo za kawaida kwenye ubongo. Hakiambukizi wala si laana. Watu 7 kati ya 10 wenye kifafa huacha kupata degedege wakitumia dawa kila siku, na wanaweza kusoma, kufanya kazi na kuishi maisha ya kawaida.

Uvimbe wa Batholini (Bartholin cyst)

Uvimbe wa Batholini (Bartholin cyst)

Uvimbe wa Batholini (Bartholin cyst) hutokea tezi ndogo zilizo pembeni ya mlango wa uke zinapoziba na kujaa ute. Uvimbe usio na maambukizi mara nyingi hauumi; ukiambukizwa huwa jipu lenye maumivu makali, uvimbe mwekundu na homa. Hutibiwa kwa kuloweka kwenye maji ya uvuguvugu, na jipu kwa kutoa usaha na wakati mwingine antibiotiki.

Phecomelia

Phecomelia

Ulemavu unaotokana na kutofanyika kikamilifu au kukosekana kabisa kwa miguu na mikono kunakochangiwa sana na matumizi ya dawa ya ukoma yenye jina la thalidomide wakati wa ujauzito.

bottom of page