Magonjwa na saratani mbalimbali
Sehemu hii utasoma kuhusu hali na magonjwa mbalimbali

Pumu ya ngozi au ukurutu (atopic eczema)
Pumu ya ngozi au ukurutu wa atopiki (atopic eczema) ni ugonjwa sugu wa ngozi unaoleta ngozi kavu, mwasho mkali na mabaka mekundu au meusi yanayokuja na kuondoka. Huanza mara nyingi utotoni na huambatana na pumu ya kifua na mafua ya mzio. Haiambukizi. Hudhibitiwa kwa mafuta laini kila siku, kuepuka vichochezi na krimu za steroidi wakati wa kupamba moto.

Vipele vya jasho (miliaria)
Vipele vya jasho (miliaria, au prickly heat) ni vipele vidogo vinavyotokea mirija ya jasho ikiziba wakati wa joto na unyevu, hasa shingoni, kifuani, mgongoni na kwenye mikunjo ya ngozi. Huleta mwasho au kuchoma kama sindano. Si hatari wala haviambukizi. Hupotea ndani ya siku chache ukiwa mahali pa baridi na ukivaa nguo nyepesi.

Kutoumbwa kwa UKE
Ni hali ya kuzaliwa ambapo uke na mara nyingi mfuko wa uzazi haujaundwa kikamilifu, huku ovari mara nyingi zikiendelea kufanya kazi na kuzalisha homoni na mayai. Uchunguzi sahihi na matibabu kama utanuzi wa uke au upasuaji inapohitajika pamoja na msaada wa kisaikolojia na ushauri kuhusu uzazi, vinaweza kumsaidia mhusika kuishi maisha yenye afya na mahusiano mazuri.

