Majibu ya maswali mbalimbali

Sikio kupiga kelele: Visababishi, Uchunguzi na Tiba
Sikio kupiga kelele (tinitas) ni hali ya kusikia sauti kama upepo, mlio, mluzi au milio ya nyuki bila chanzo cha sauti cha nje. Mara nyingi huhusiana na mafua, kuziba kwa sikio, au matatizo ya mfumo wa kusikia na huhitaji tathmini ya kitaalamu endapo hudumu muda mrefu.

Magonjwa yanayochangia kutoshika mimba: Mwongozo kwa wanawake
Magonjwa mbalimbali yanaweza kuathiri uovuleshaji, mirija au mfuko wa uzazi na hivyo kuchangia kutoshika mimba kwa wanawake, hata bila dalili za wazi. Uelewa wa mapema, uchunguzi sahihi na matibabu ya kitaalamu huongeza kwa kiasi kikubwa nafasi ya kupata ujauzito.

Je katikati umri wa miezi 4 na wiki 2 naweza kuanza kumpa mtoto uji?
Haipendekezwi kuanza kumpa mtoto uji au chakula chochote cha nyongeza akiwa na miezi 4 na wiki 2. Umri salama, uliothibitishwa kitaalamu, ni miezi 6 kamili isipokuwa katika mazingira maalumu ya kitabibu ambayo daktari ameshauri vinginevyo.

Lishe ya nyongeza kwa mtoto baada ya kuzaliwa: Ianze lini na apewe nini?
Lishe ya nyongeza inapaswa kuanza miezi 6 kwa kutoa vyakula vyenye virutubisho vingi, salama, na vilivyoboreshwa kulingana na umri wa mtoto. Kuchelewa au kufanya vibaya kunaweza kusababisha utapiamlo, udumavu, na matatizo ya ukuaji wa ubongo.

Hedhi yenye damu kidogo na maumivu makali: Visababishi, Uchunguzi na Tiba
Hedhi yenye damu kidogo na maumivu makali inaweza kusababishwa na mabadiliko ya homoni, matatizo ya kizazi, au hali za kiafya kama endometriosis. Uchunguzi wa kina na tiba ya mapema ni muhimu kuhakikisha afya ya uzazi na ubora wa maisha.

Vidonda vinavyouma Ukeni: Dalili, Visababishi na Matibabu
Vidonda vinavyouma ukeni mara nyingi husababishwa na maambukizi kama Herpes, chankroidi(pangusa), kaswende, fangasi au athari za kemikali na majeraha ya uke. Utambuzi wa mapema na matibabu sahihi ni muhimu ili kuzuia maumivu kuongezeka, maambukizi kurudia na madhara ya muda mrefu.

Kaswende isiyopona: Vipimo na Hatua Muhimu za Kuchukua
Kaswende isiyopona hutokea pale maambukizi ya Treponema pallidum hayaitikii dawa au mtu huambukizwa tena kutokana na kutozingatia hatua sahihi za tiba na ufuatiliaji. Vipimo maalumu kama VDRL/RPR, TPHA na uchunguzi wa maji ya uti wa mgongo ni muhimu ili kubaini chanzo na kuongoza matibabu sahihi.





