top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY-Clinic

 

Miwasho sehemu za siri(ukeni)

 

Miwasho sehemu za siri/Ukeni huweza kusababisha  mwanamke kujihisi vibaya sana na haswa akiwa sehemu za watu kwa sababu hali hii humlazimu ajikune au aondoke kwenye shughuli alokuwa anafanya akapate kujikuna maeneo yanayowasha. 

 

Miwasho ukeni huashiria kuna maambukizi au kitu fulani kigeni kimeingia sehemu hizo na hivo lengo la makala haya ni kuzungumzia vitu na maambukizi yanayosababisha miwasho ukeni

 

Nini husababisha miwasho Ukeni?

 

Maambukizi mbalimbali yanaweza kusababisha miwasho ukeni kama;

 • Maambukizi ya bakiteria

  • maambukizi ya bakiteria maeneo haya huweza kusababisha miwasho pamoja na kuhisi kama unaungua , kutoa harufu mbaya kama samaki aliyeoza na kutoa uchafu ukeni wa rangi tofauti

 • Magonjwa ya zinaa

  • Kisonono, kaswende, trichomoniasis, virusi vya herpes na maoteo sehemu za siri yanayosababishwa na virusi vya human papilloma

 • Mambukizi ya fangasi ukeni- wanawake wa 3 kati ya wa 4hupata  maambukizi haya maishani mwao. Maambukizi haya hutokea pale ambapo fangas hawa wamezaliana kupitiliza kwa Kuchangiwa na mambo mengi kamvile kinga ya mwili kushuka au kutumia dawa za antbiotik ambazo huua bakteria walinzi

Vihatarishi ni vya miwasho ukeni

 • Kufanya mapenzi na mtu mwenye fangasi (ingawa fangas huwa sio ugonjwa wa zinaa)

 • Ujauzito

 • Kinga ya mwili kuwa chini

 • Kutumia madawa ya antbakteria (ambayo huua bakteria walizi wa uke na hivyo kuwapa nafasi fungus kuzaliana na kutawala) Wanawake wote wapo hatarini kupata maambukizi haya kama kinga zao za mwili zipo chini, mbali na kuwashwa mgonjwa hutoa majimaji mazito na meupe au kama maziwa ukeni, lakini pia huweza kubadilika na kuwa mepesi yanayotoa harufu kiasi

 • Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango

 • ugonjwa wa Kisukari

 • Msongo wamawazo

 

 • Komahedhi - kutokana na mabadiliko katika mfumo wa vichochezi mwili, wanawake waliokoma kuona siku zao za mwezi mara nyingi kichochezi cha estrogeni huwa chini sana na kusababisha uke kuwa mkavu na kuta kuwa nyembamba na hivo huleta miwasho sehemu hizi- pia kwa baadhi ya wanawake wanapokuwa wananyonyesha tatizo hili linaweza kutokea pia kwa sababu hiyo

 • Kemikali mbalimbali zilizo kwenye sabuni, mafuta ya cream au mafuta mengine , baadhi ya pedi, karatasi za kujifutia unapotoka chooni.

 

Matibabu  ya miwasho ukeni?

 

Matibabu ya miwasho ukeni yapo ila hutegemea sababu ni nini, ikiwa umetumia dawa flani au mafuta yanayosababisha miwasho basi ni vema kuacha kutumia dawa hiyo, miwasho na miunguzo itaisha yenyewe baada ya siku chache.

 

Ikiwa miwasho na michomo inaendelea au uchafu unatoka ukeni basi ni vema kuonana na dakitari ili ufanyiwe uchunguzi wa sehemu hizi na upatae matibabu sahisi

 

Kukutana na madaktari wetu wasiliana nasi kwa kuingia kwenye akaunti yako, kama hujafungua akaunti unaweza anza sasa

Imechapishwa 22.11.2020

bottom of page