top of page

Kinga ya magonjwa ya moyo | ULY CLINIC

Updated: Dec 11, 2020


Kwa ujumla, maisha yanayozingatia kanuni za afya hupunguza kwa zaidi ya asilimia 80 ya magonjwa ya mishipa ya moyo na asilimia 50 ya kiharusi kitokanancho na kukosa damu sehemu fulani ya ubongo kitaalamu-ischemic sroke(taarifa kutoka hervard urniversity).

Kuzuia magonjwa ya mishipa ya moyo na kiharusi, inahitajika kuzuia vihatarishi vinavyoweza kusababisha magonjwa hayo.Vihatarishi hivi ni vema vikaepukwa mapema mtu anapokuwa anakuwa kwa sababu mabadiliko mengi yanatokea kwenye mwili wa binadamu kwa muda mrefu yanayoweza kumuweka hatarini kupata magonjwa haya. Mfano tafiti zinaonyesha kwamba magonjwa ya mishipa ya moyo na kiharusi kwa kiasi kikubwa huweza kusababishwa na kuganda (hardening) kwa mishipa ya damu ya sehemu husika (moyo au ubongo) mgando huo hutegemea kiwango cha mafuta kwenye damu, mabadiliko haya huwa sio ya siku mbili au tatu, huchukua miaka mpaka mtu kuja kupata migando (hardening) hiyo.


Hivyo tahadhari ya mda mrefu kama vile mtoto anapoendelea kukua anatakiwa kuandaliwa vyema kwenye masuala ya chakula ili aishi katika kanuni za afya na apate matokeo mazuri ya afya yake hata kipindi hiki cha umri wa kati au uzeeni. Hivyo kinga ya awali inahitajika katika kuzuia magonjwa mengi yasiyoambukizwa.


Ni kanunu gani upasaswa kuzingatia?


Kwa ushauri zaidi unaweza wasiliana na daktari wako au madaktari wa uyclinic. Endelea kusoma makala zetu kupitia tovuti hii


Bonyeza kusoma pia kuhusu makala ya moyo kwenda kasi, kuhisi mapigo ya moyo na kinga na magonjwa ya moyo
Usisahau kuwashirikisha watu uwapendao kupakua app ya ULY CLINIC


Karibu ULY CLINIC kwa tiba na ushauri.

102 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page