top of page

Imeandikwa na ULY CLINIC

Bofya hapa kutumia kikokoteo cha kukuambia tarehe yako ya kijifungua, tarehe ya kupata mimba na umri wa ujauzito, au endelea kusoma makala na kukokotoa tarehe yako mwishoni wa makala hii

Unawezaje kufahamu tarehe yako ya kujifungua?

Mama mwenye ujauzito unatakiwa kufahamu tarehe yako ya kujifungua ili uweze Kupanga na kujiandaa kabla ya kujifungua. Endapo wewe na mpenzi wako mnafahamu tarehe ya kujifungua itawapa muda mzuri wa ninyi kupanga unataka kujifungulia wapi hivyo kufanya maandalizi muhimu ya kipesa na watu ambao wataambatana nawe kukupa msaada kabla ua baada ya kujifungua. 

 

Umri wa ujauzito ni miezi au wiki ngapi?

Wastani wa kipindi cha ujauzito ni siku 280 ama wiki 40 kamili kwa binadamu.

Njia gani hutumika kukokotoa tarehe ya kujifungua?

 

Ili  kujua tarehe yako ya kujifungua, njia inayotumika kujua tarehe yako inaitwa Naegele's rule.

Njia hii hutumika mara nyingi kwa mwanamke mwenye mzunguko usio badilika badilika sana na unachukulia mwanamke anaona hedhi baada ya siku 28  na katikati ya mzunguko wake ni siku 14. Kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 35 siku yake ya katikati ni siku ya 21

 

 

Tarehe ya matazamio hutambuliwa kwa, kwanza kujua tarehe yako ya mwisho ya siku ya kwanza kuaona damu ya mwezi. Kisha;

  • Ongeza 7 kwenye tarehe

  • Jumlisha 9 , ama  toa 3 kwenye mwezi kwa mzunguko wa siku  28 (Jumlisha 9 endapo mwezi upo chini ya miezi 4 au toa tatu kama mwezi upo zaidi ya miezi 3)

  • Ongeza 0 tu kwenye mzunguko wa siku  21

  • Ongeza 14 kwenye tarehe kwa mzunguko wa siku 35

Mfano kama mwanamke mara ya mwisho kuona siku zake ni tarehe 21/3/2008 hivyo tarehe ya matazamio ni

                       

          siku   mwezi   Mwaka   

           21        3       2008

         + 7       +9

           28       12      2008

 

Kama siku yake ya mwisho kuona damu ni 21/5/2008

        siku  mwezi    mwaka

         21       5         2008

        + 7      -3

         28        2         2009

 

Na ikiwa mwanamke ameona siku yake ya mwisho tarehe 25/6/2015 tarehe yake ya matazamio ni

 

      siku  mwezi    mwaka

        25       6           2015

       +7       -3 

        2         3           2016

Kama hujaelewa mahesabu haya tumia kikokoteo chini ya maelezo ya mada hii

Endapo umesahau tarehe ya mwisho kuona damu unifanye nini ili kufahamu tarehe yangu ya kujifungua?

Endapo umesahau tarehe yako ya kwanza mara ya mwisho kuona damu ya  hedhi, unaweza kukisia tarehe hiyo kwamba ilikuwa ni mwanzoni, katikati au mwishoni mwa mwezi kisha kuweka tarehe hiyo kwenye kikokoteo cha tarehe ya kujifungua chini ya makala hii.  Kumbuka endapo ulisahau tarehe yako ya mwanzo kuona damu ya hedhi njia hii inakuwa si sahihi zaidi.

 

Njia nyingine unaweza kuitumia ni kwa kupimwa ukubwa wa  tumbo lako la uzazi ili kujua umri wa mimba na tarehe ya kujifungua au kutumia kipimo cha ultrasound ambacho huwa sahihi zaidi haswa kwenye ujauzito wenye umri chini ya miezi minne.

EDD

Tumia kikokoteo chini ya maelezo kujua tarehe yako ya kujifungua.

 

Maelezo kabla ya kujaza

Weka chagua mwezi, tarehe na mwaka wa siku ya kwanza ya kuanza hedhi yako ya mwisho, kisha chagua idadi ya Siku za mzunguko wako wa hedhi moja hadi nyingine( mfano ni siku 22, 26, 28, 30, 32 n.k). Baada ya kujaza bofya Calculate na soma majibu kwa kulinganisha na aya zilizoandikwa hapo chini

Maelezo kuhusu majibu ya kikokoteo cha tarehe ya kujifungua hapo juu baada ya kuingiza taarifa zako na kubofya 'calculate'

Utakapotumia kikokoteo hicho hapo juu, utapata majibu kwenye  aya tatu hadi nne ya majibu ambayo yameandikwa kwa lugha ya kiingereza. Majibu yako yaliyotokea yatafsiri hapa chini kwa kufananisha  aya ya kwanza hadi ya tatu au nne zilizotokea baada ya kubofya 'calculate'

Aya ya kwanza inamaanisha kwamba, endapo hujuapata mimba utaingia hedhi inayofuata kuanzia tarehe ilioonyeshwa kwenye aya ya kwanza.

Aya ya pili inamaanisha kuwa endapo huna ujauzito tarehe yako ya siku za hatari inatarajiwa kuwa kati ya tarehe zilizoorodheshwa kwenye aya ya pili.

Aya ya tatu unamanaisha, endapo umepata ujauzito tarehe yako ya matazamio ya kujifungua itakuwa kwenye tarehe hiyo iliyotajwa kwenye aya ya tatu.

Aya ya nne ambayo wakati mwingine haionekani kwenye baadhi ya tarehe utakazoingiza inamanisha, endapo umepata ujauzito, ujauzito wako utakuwa na umri wa wiki zilizotajwa hapo kwenye aya ya nne.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa elimu na ushauri zaidi baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa kupiga simu au bofya 'Pata Tiba' kupitia neno Pata Tiba chini ya tovuti hii. au Bofya hapa

Imeboreshwa, 23.01.2021

Rejea za mada hii,

  1. JOHN HOPKINS https://www.hopkinsmedicine.org/health/wellness-and-prevention/calculating-a-due-date. Imechukuliwa 21.02.2020

  2. Modified Naegele’s Rule for Determination of the Expected Date of Delivery Irrespective of the Cycle Length.

  3. PDF. http://applications.emro.who.int/imemrf/med_j_cairo_univ_1994_62_1_39.pdf.Imechukuliwa 21.02.2020

  4. Maswali na majibu kutoka kwa wateja wa

  5. ulyclinic. https://www.ulyclinic.com/forum/majadiliano-na-wataalamu/nawezaje-kufahamu-tarehe-yangu-ya-kujifungua-endapo-nimesahau-tarehe-ya-mwisho-kuona-damu-ya-hedhi. Imechukuliwa 27.05.2020

bottom of page