top of page

Vipimo vya Msingi mama kufanya wakati wa ujauzito

 

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

​

Hakuna mama anayetaka kujifungua mtoto asiyefanana na binadamu wengine, ni dhahiri kwamba kama yupo basi atakuwa anatatizo katika akili yake na anahitaji ushauri. Yapo magonjwa mengi yanayoweza kuzuilika endapo mama atafanya vipimo mapema zaidi kabla na baada ya kupata ujauzito. Wakati wa wiki za kwanza za ujauzito, hatua za awali za utengenezaji wa vioungo mbalimbali vya mtoto hufanyika hasa kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito. kipindi hiki mama anatakiwa kuwa makini nacho ili kuweza kumkinga mtoto na madhara mbalimbali kama vile kuzaliwa na ulemavu wa viungo vya mwili(macho, moyo,mikono na miguu na kichwa) kwa kuzingatia kanuni mbalimbali zilizowekwa

 

vipimo gani vinatakiwa kufanyika kabla ya ujauzito na ni kwanini ufanye?

 

  • kipimo cha mkojo kuangalia maambukizi ya UTI, kichocho

kipimo cha damu kuangalia maambukizi ya kaswende, virusi vya ukimwi, toxoplasmosis, virusi vya homa ya ini, kirusi vcha CMV ugonjwa wa rubella

  • kipimo cha malaria

  • kipimo cha shinikizo la damu

  • kipimo cha sukari

 

 

Vipimo gani vinatakiwa kufanyika wakati wa ujauzito na kwanini ufanye?

 

  • kipimo cha ultrasound- ama mionzi sauti-kugundua hali na uhai wa mtoto(mtoto mlemavu wa miguu mikono kichwa ama moyo, kuangalia kama mtoto anaishi na kupima umri wa mtoto. Ni vema mama akapima kipimo hiki kwa mara ya hasa pale anapokuwa na ujauzito chini ya miezi mitatu na baada ya hapo anaweza kufanya kipimo hiki mara mbili ama tatu kama akiweza.

​

ULY Clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchuku hatua yoyote ile inayohusu afya yako.

​

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa elimu zaidi na Tiba kwakubonyeza Pata Tiba au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.

​​

Bonyeza kusoma makala zingine zaidi kuhusu;

​

Vipimo vya kufanya wakati wa ujauzito
bottom of page