top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY-Clinic

 

 

Tatizo la Goita

 

Katika mwaka 1656, Thomas Wharton alielezea asili tofauti ya kile alichokiita tezi ya shingo ama tezi ya thyroid na kuitofautisha na tezi koo, kwa sababu muundo huo ulikuwa ukifahamika kwamba  tezi ya thyroid ni tezi ya koo , tokea enzi za mzungu anayeitwa Andreas Vesalius katika karne ya 16. Ilikuwa takribani miaka 200 na  zaidi kabla utambuzi wa  tezi shingo kutambuliwa ama kuelezewa.

 

Mtu mzima ana tezi shingo ama tezi ya thyroid yenye uzito wa gramu 10 hadi 25, tezi shingo ina sehemu kuu 2 na sehemu hizi zimeshikamanishwa na ukuta unaoitwa isthmus. Karibia asilimia  50 ya tezi ya thyroid huwa inaonyesha kuwa  na kijioteo cha tezi katikati ya isthmus na kinaumbo la piramidi(pembetatu).

 

Goita ni tezi ya thyroid iliyokuwa kupita kiasi, inaweza kuwa imesambaa kwa mapana ama kuwa na manundu manundu. Goita inaweza kukua na kufika mabegani ama wakati mwingine bila hata kuonekana kukua mbele ya shingo ama kuonekana kabisa

 

Kwa sababu ya mahusiano ya kianatomia(maumbile) kati ya tezi shingo, kolomeo la hewa, koo na mishipa ya fahamu ya laryngeal ya juu na ya chini(inferior and superior laryngeal nerve) na  mrija wa kupitisha chakula, kukua kwa tezi hii kunaweza kusababisha mgandamizo kwenye maeneo hayo na kuzalisha dalili mbalimbali zinazotokana na migandamizo kwnenye maeneo husika. Uzalishaji wa homoni katika goita unaweza kuwa wa kiasi cha kawaida ama kuzalishwa kwa wingi, hapa tunaita goita lenye sumu ama toxic goita

​

Visababishi

​

Sababu zinazoweka kusababisha upungufu wa homoni ya thyroid ni;

  • matatizo ya kuzaliwa ya shida katika uzalishaji wa homoni ya thyroid,

  • upungufu wa madini chuma mwilini au

  • kula vyakula vinavyosababisha kukua kwa tezi hii.

  • Ujauzito

  • Goita pia inaweza kuota kutokana na dawa zinazopingana na kazi za TSH. Uzalishaji wa TSH unawez kuongezwa na kinga za mwili dhidi ya TSH,

  • ukinzani wa tezi pituitary kutambua kiwango cha homoni ya thyroid,

  • saratani au vimbe za tezi ya pituitary pamoja na hypothalamus na saratani inayozalisha kwa wingi homoni ya gonadotropin(HCG) inayotolewa wakati wa ujauzito

​​

Mahusiano ya uzalishaji wa Homoni ya Thyroidi na Ukuaji wa Goita

 

Uzalishaji wa tezi ya thyroid huongozwa na homoni chochezi ya thyroid ikijulikana kwa kifupi kama TSH, homoni TSH huzalishwa katika tezi ya pituitary iliyopo kichwani chini ya ubongo, na uzalishwaji huu wa TSH pia husimamiwa na homoni inayoruhusu kutolewa kwa thyroid inayoitwa thyrotropin releasing hormone ama TRH kwa kifupi ikitoka katika tezi ya hypothalamus. TSH inaruhusu kuku , na kufanya chembe za tezi hii kuwa na sifa zake za asili, pia inaruhusu uzalishaji wa homoni au kichochezi cha thyroid.

 

Thyrotropin hufanya kazi katika milango ya tezi ya thyroid. Vichochezi vya thyroid huzalishwa katika kitendo cha kuunganisha madini chuma na protini inayoitwa tyrosine ndani ya tezi hii ya thyroid. Madini chuma husafilishwa kutoka katika damu na kuingi katika tezi hii kwa milango maalumu iliyopo kwenye chembe hai za thyroid na hivyo kufanya kiwango cha madini chuma ndani ya tezi hii kuwa mara 20 zaidi ya kile kilichopo katika damu. Usafilishaji wa madini chuma hulekebishwa na homoni ya TSH.

 

Uzalishaji wa homoni za thyroid ukiwa unatosha basi kunataarifa hutumwa kawenye tezi ya pituitary na hivyo husitisha uzalishaji wa homoni ya TSH. Kuhalibiwa kati ya mzunguko wa homoni hizi mbili za TSH na TRH kunasababisha kubadilika kwa kazi na umbo la tezi ya thyroid. Uchochezi kazi za TSH na TRH kama kutokana nahomoni inayozalishwa wakati wa ujauzito inayoitwa Gonadotropin, husababisha kukua kwa goita. Kama kukiwa na magonjwa, ama michomo ama saratani za awali au zilizosambaa kwenye tezi hii husababisha tezi kupata vinundu na kukua umbo.

 

Upungufu wa uzalishaji wa homoni ya thyroid ama kupungua kutokana na kuacha kunywa dawa huongeza uzalishaji wa homoni ya TSH. Kuongezeka kwa uzalishaji wa homoni ya TSH husababisha kuongezeka kwa namba ya chembe na umbo la chembe za tezi hii zinazohusika katika uzalishaji wa homoni ya thyroid, madhumuni ya ukuaji huu ni kurekebisha uzalishaji wa homoni ya thyroid kuwa kma kawaida. Kama tendo hili likiendelea kwa muda inasababisha kutokea kwa goita.

​

Data za kidunia(epidemiolojia)

                                                                                   

Kidunia, sababu kuu inayosababisha goita ni uoungufu wa madini joto, inakadiliwa kwamba tatizo hili la goita linawaathiri watu zaidi ya 200 kati ya watu 800 walio na upungufu wa madini joto kutoka kwenye chakula. Kisababihi kikuu cha goita katika Amerika ni ugonjwa wa kinga za mwili kupambana na mwili wenyewe au autoimmune disease

 

Madhara na vifo

​

Goita nyingi huwa hazisababishi matatizo, husababisha kuondoa ulembo tu kutokana na uvimbe shingoni. Kifo au madhara yanaweza kutokana na mgandamizo wa uvimbe huu katika maeneo jirani, kubadilika kuwa saratani, kwango kikubwa cha homoni ya thyroid au kiwango kidogo.

 

Jamii

Hakuna jamii Fulani inayopata san atatizo hili kuliko nyingine

​

Jinsia

wanawake wanapata goita mara 4 zaidi kuliko wanaume

​

Umri

kadri mtu anavyoongezeka umri, kutokea kwa goita hupungua, lakini kuwa na viuvimbe kwenye tezi shingo huongezeka kwa jinsi umri unavyoongezeka

​

Dalili za goita

 

Goita inaweza kujitokeza na dalili tofauti, kama zifuatazo

 

  • Uvimbe mbele ya shingo

  • kutopumua ama kuvuta pumzi vema

  • kutoa miruzi ama sauti kubaadilika

  • kushindwa kumeza chakula

  • kusikia joto sana mwilini ama kupata njaa sana

  • kusikia baridi na

  • Dalili zingine za wingi ama upungufu wa homoni ya thyroid mwilini

 

Kama una maswali kuhusu matibabu basi tupigie simu ama tutumie email/message katika namba zetu hapo chini ya website, karibu ugonjwalughayetu clinic kwa matibabu

​

Imeboreshwa mara ya mwisho 07.07.2020

​

ULY Clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchuku hatua yoyote ile inayohusu afya yako.

​

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa elimu zaidi na Tiba kwakubonyeza Pata Tiba au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.

​​

Bonyeza kusoma makala zingine zaidi kuhusu;

​

Goita ujauzitoni
bottom of page