top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

Huduma za klinic  kwa mama majawazito

 

Huu ni mpango wa kuwapa umakini wa kitabibu kwa  wamama kipindi cha ujauzito  na kabla ya kujifungua

 

Kwanini kuwa na huduma hii ya kliniki kwa kina mama?

 

Madhumuni makuu ni

 

 • Kuzuia, kugundua na kutibu na kusaidia kuzuia jambo au mambo yanayodhuru ujauzito na hivyo afya ya mama na mtoto aliye tumboni.

 • Kutoa ushauri, kuwapa uhakika, kutoa elimu na msaada kwa mama na familia yake

 • Kutatua matatizo madogodogo ya ujauzito

 

Mgonjwa atahitaji kupewa maelezo kuhusu dalili au mambo mbalimbali ya mabadiliko ya mwili yanayotokea kipindi cha ujauzito ili ajiandae kisaikolojia kuhusu madabiliko hayo

 

 • Kupimwa afya kwa ujumla ili kujua magonjwa yanayoweza kumdhuru mama na mtoto aliye tumboni

 

Ni Faida zipi za kuhudhuria klinic ya Wajawazito?

 

Mama anapohudhuria klinic anaweza kupata faida zifuatazo;

 

 • Kugunduliwa na kutibiwa kwa upungufu wa viinirishe mwilini

 • Kutibiwa kwa magonjwa ya malaria, minyoo, na kutibiwa tatizo la shinikizo la juu la damu

 • Kugunduliwa kwa vihatarishi vitakavyoweza kudhuru ama kuhatarisha afya ya mama na mtoto

 • Kupewa kinga dhidi ya upungufu wa damu na tetenusi

 • Kuwaelimisha na kuwataarifu wamama na familia kuhusu lini na wapi watafute msaada wa kiafya

 • Kumsaidia mama kupanga muda na mahali pa kujifungulia ili kuepuka madhara wakati wa kujifungua

 • Ushauri nasaha na Kupima kwa hiari maambukizi ya ukimwi

 • Elimu kuhusu uzazi wa mpango na namna ya kunyonyesha

 • Kuwapa moyo  kuhusu ujauzito unavyoendelea, mama familia na ndugu

Wakati gani mama mjamito uanze kuhudhuria kliniki ?

 

Shirika la afya duniani WHO (World Health Organization) limeshauri mama kwenda klinic kuazia mara nne katika kipindi chote cha ujauzito ili kufanyiwa vipimo na matibabu kwa Afya yamama na mtoto kwa ujumla 

 

 • Kwa mara ya kwanza kabisa mama anatakiwa aende klinic kuazia wiki 12(miezi mitatu) za ujauzito lakini zisifuke wiki 16 bila kwenda kwa mara ya kwanza

 • Mara ya pili anatakiwa ahudhurie clinic akiwa na ujauzito wa wiki 20 - 24

 • mara ya 3 anatakiwa kuhudhuria klinic akiwa na ujauzito wa wiki:  28 - 32

 • Mara ya 4 anatakiwa kuhudhuria klinic akiwa na ujauzito wa wiki  36 

 • Mara ya tano(Hiari) akiwa na ujauzito wa wiki 40

 

Hata hivyo  Royal College of Obstetricans and Gynaecologists wanashauri wanawake wahudhurie klinic angalau mara 5 katika kipindi chote cha ujauzito, mahudhurio hayo ni kama ifuatavyo;

 

 • Mara ya kwanza wiki ya  12

 • Mara ya pili wiki ya 20

 • Mara ya tatu wiki ya 28-32

 • Mara ya nne wiki ya  36 na

 • Mara ya tano wiki ya 40-41

ULY CLINIC inakushauri siku zote ufuate ushauri wa daktari kabla ya kuchukua uamuzi wowote ule wa kiafya.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri zaidi kuhusu masuala ya uzazi na tiba kwa kutumia nambaz a simu chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa, 07.07.2020

Bonyeza kusoma makala zingine zaidi kuhusu;

Huduma za kliniki
bottom of page