top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

 

Ujauzito hatari

 

Utangulizi

​

Ujauzito hatari ni ule ambao  unaongeza nafasi ya mimba kutoka, mtoto kufia tumboni, kuzaa njiti, mtoto kudumaa tumboni, magonjwa kwa kichanga, matatizo ya kiuumbaji, kudumaa ubongo na madhara mengine. Baadhi ya mambo yanayochangia kama kula sumu zinazoingilia uumbaji wa mtoto katika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito huhusiana na ujauzito hatar. Mamabo mengine ni kama maji katika chupa ya uzazi haswa yakiwa mengi au kidogo.

 

Kwa kawaida asilimia 10 hadi 20 ya wanawake wenye ujauzito huwa na ujauzito hatarishi na nusu ya matatizo na vifo kwa mama au mtoto vinavyotokea kwenye ujauzito huhusiana  na ujauzito hatarishi. Ingawa uchunguzi unatakiwa kufanywa mara kwa mara kwenye ujauzito kipindi chote, madhara na vifo huweza kutokea kipindi cha uchungu na kujifungua, hivyo uchunguzi na umakini unatakiwa kufanyika kipindi chote cha ujauzito.

 

Kutambua ujauzito hatarishi huweza kusaidia hatua ya kwanza kwenye matibabu na kuzuia madhara kwa sababu hatua za matibabu zitafuata kupunguza hatari kwa mtoto na mama endapo mtaalamu atajua madhara ya kihatarishi ulichonacho.

 

Mambo yanayohusiana na mimba hatarishi

  • Sababu za kiuchumu

  • Umasikini

  • Kutokuwa na ajira

  • Kutokuwa na huduma kama za bima ya afya

  • Kutopatikana kwa huduma za kliniki ya wajawazito kwa karibu au kutokuwepo kabisa

 

Sababu za kitamaduni

  • Kutokuwa na elimu au kuwa na elimu ndogo

  • Msimamo mbaya kuhusu huduma za kiafya

  • Kutopata huduma za kliniki au kutohudhuria kabisa

  • Kuvuta sigara, kunywa pombe, na kutumia madawa ya kulevya

  • Umri chini ya miaka 20 au zaidi ya mika 35

  • Kutokuwa kwenye ndoa

  • Mimba za karibu karibu

  • kutokuwa na kundi saidizi(mume, familia, dini)

  • msongo wa mawazo

  • kuwa mtu jamii ya rangi nyeusi

 

Sababu  za kibiolojia

  • Historia ya kuwa na njiti au uzito mdogo kwenye ujauzito uliopita

  • Uzito mdogo kulinganisha na urefu

  • Kuongezeka uzito kidogo sana kipindi cha ujauzito

  • Kuwa mfupi

  • Lishe duni

  • Ugonjwa wa kutokwa damu

  • Uzito kidogo wa mama

  • Magonjwa ya kurithi(matatozo ya kuzaliwa nayo ya uchakatuaji katika seli)

 

Sababu za uzazi

 

  • Historia ya kujifungua kwa upasuji ujauzito uliopita

  • Tatizo la ugumba

  • Mimba za kupandikiza kisayansi

  • Ujauzito uliopitiliza umri

  • Uchungu iliopitiliza mda

  • Mtoto aliyepita kua na mtindio wa ubongo,kudumaa akili na matatizo ya kuumbaji

  • Mtoto kulala vibaya

  • Mimba yenye mtoto zaidi ya mmoja- mapacha

  • Kifafa cha mimba

  • Kutokwa na damu(kondo kujiachia au kujipandikiza karibu na shingo ya uzazi)

  • Uzazi wa kwanza au zaidi ya 5

  • Umbile bovu la kizazi au shingo ya uzazi

  • Ugonjwa kwa kichanga

  • Mtoto kukua vibaya/kusiko kawaida

  • Uchungu kabla ya mda kutimia

  • Kiwango kidogo au kikubwa cha kawaida homoni ya kuwadia alpha fetoprotein

 

Magonjwa

  • Kisukari

  • Shinikizo la juu la damu

  • Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo

  • Magonjwa ya autoimmune

  • Ugonjwa wa kuishiwa damu wa sickle cell

  • Maambukizi ya TOCHI (toxoplamsa, vimelea wengine, rubella, cytomegalovirus, kirusi cha surua)

 

Kama unavihatarihi vya hapo juu basi onana na daktari wako ili mpanga aina ya matibabu na uchunguzi unaotakiwa kufanya mara kwa mara ili kuzuia madhara yanayowezakuzuilika au wasiliana na madaktari wetu popote pale ulipo kupitia namba zetu na utasaidia kwa ushauri na matibabu.

 

Imeboreshwa mara ya mwisho 07.07.2020

​

ULY Clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchuku hatua yoyote ile inayohusu afya yako.

​

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa elimu zaidi na Tiba kwakubonyeza Pata Tiba au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.

​​

Bonyeza kusoma makala zingine zaidi kuhusu;

​

Ujauzito hatari
bottom of page