top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD, Dkt. Adolf S, MD

Alhamisi, 26 Agosti 2021

Kipindi cha kwanza cha ujauzito

Kipindi cha kwanza cha ujauzito

Kipindi cha kwanza cha ujauzito huanza baada ya utungisho wa yai ndani ya mirija ya uzazi na kuisha baada ya ujauzito kumaliza wiki 12. Kipindi hiki uumbaji wa kichanga na ogani zake hufanyika na huweza athiriwa kwa chakula pamoja na dawa unazotumia.


Mwishoni mwa wiki ya 4


Mwishoni mwa wiki 4 baada ya utungisho vitu vifuatavyo huwa vimeshatokea


  • Utengenezaji wa ogani kuu

  • Mtoto huonekana kama kijusi

  • Mrija wa fahamu huwa umeshatengenezwa ambao baadae hubadilika kuwa ubongo na uti wa ngongo

  • Macho na masikio huanza kutengenezwa

  • Kuanza kuchomoza kwa mikono na miguu

  • Moyo huanza kufanya kazi


Wiki ya 8 baada ya utungisho


Viungo vyote vikuu huwa vimeshatengenezwa na huendelea kukua kiumbo na kikazi viungo hivyo ni pamoja na mfumo wa mkojo, mfumo wa fahamu, mfumo wa mme’nyengo wa chakula na mfumo wa moyo na mishipa ya damu.


  • Kijusi huanza kubadilika kuwa sura ya binadamu, kichwa huw akikubwa zaidi ya kiwiliwili

  • Mdomo wa mtoto hutengenezwa

  • Macho, pua, mdomo na masikio huanza kupata umbile lake asili

  • Mikono na miguu huweza kuonekana kirahisi

  • Vidole vya mikono na miguu huwa na utando katikati yake( kama bata) bado lakini huweza kuonekana

  • Mifupa na taya la mtoto hukua kwa haraka

  • Kijusi huwa anacheza tumboni lakini mama hawezi tambua


Baada ya wiki nane kutimia, yai lililochavushwa huitwa kijusi, licha ya kuwa kidogo sana ( kati ya sentimita 1.27 hadi 2.54), kijusi hiki huwa tayari kina ogani zote kubwa.


Wiki ya 9 hadi 12


  • Wiki ya 9 hadi 12 mambo yafuatayo huonekana/kutokea

  • Viungo nje ya mwili wa kichanga huendelea kukua

  • Kucha za vidole vya mikono na miguu hutokea

  • Kope za macho hutengenezwa

  • Mtoto huongeza uchezaji

  • Mikono na miguu humalizika kutengenezwa

  • Sanduku la sauti huanza kutengenezwa kutoka kwenye trakea


Licha ya viungo vyote vya kijusi kuwa vimeshafanyika kichanga anapofikisha wiki 12, kichanga huyu huwa hana uwezo wa kuishi nje ya tumbo la mama


Mambo muhimu ya kufanya kipindi hiki

Kipindi hiki kwa kwanza cha ujauzito kwa kuwa ni muhimu, unatakiwa kuhudhuria kliniki ili kufanyiwa mambo muhimu kwa afya yako na kijusi tumboni;


Kuchukuliwa historia ya afya yako mfano kuangaliwa kama una magonjwa ya shinikizo la juu la damu, upungufu wa damu, kisukari, mzio, seli mundu, magonjwa ya kijeni n.k


  • Kuulizwa dawa unazotumia kwa lengo la kufahamu na kukubadilishia kama zina madhara kwa kijusi

  • Kuulizwa historia yako ya uzazi ikiwa pamoja na ujauzito zilizopita kwa lenngo la kukgundua na kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza. Historia inahusisha, kujifungua kabla ya wakati, mimba kutoka, njia uliyojifungua ujauzito uliopita, mimba ulizotoa, historia ya hedhi yako n.k

  • Kupewa elimu kuhusu lishe, mazoezi na dawa gani utumie na kuepuka wakati wa ujauzito, utapewa elimu ya kuacha kunywa pombe na kutumia dawa zingine za kulevya pia.


Tiba zinazoathiri uumbaji wa ogani za kijusi

Madhara ya dawa au tiba zinazoweza kuathiri uumbaji wa ogani za kijusi na hivyo kupelekea kuzaliwa na ulemavu wa ogani mbalimbali( mfano moyo, miguu, mikono, ubongo, mapafu n.k) ni;


Dawa

  • Benazepril (Lotensin)

  • Captopril (Capoten)

  • Enalapril (Vasotec)

  • Fosinopril sodium (Monopril)

  • Lisinopril (Zestril, Prinivil)

  • Lisinopril

  • Hydrochlorothiazide (Zestoretic, Prinzide)

  • Quinapril (Accupril)

  • Ramipril (Altace)

  • Isotretinoin (Accutane, Retin-A)

  • Pombe

  • Testosterone

  • Tetracycline (Achromycin)

  • Doxycycline (Vibramycin)

  • Streptomycin

  • Warfarin (Coumadin)

  • Phenytoin (Dilatin)

  • Valproic acid (Depakene, Valprotate

  • Trimethadione (Tridione)

  • Paramethadione (Paradione)

  • Carbamazepine (Tegretol)

  • Lithium (Eskalith, Lithob)

  • Methotrexate (Rheumatrex)

  • Aminopterin

  • Penicillamine (Ciprimene, Depen)

  • Thiouracil/propylthiouracil

  • Carbimazole/methimazole

  • Cocaine

  • DES (diethylstilbestrol)

  • Thalidomide (Thalomid)

  • Mionzi kama vile mionzi ya tiba ya saratani, X-ray n.k

  • Magonjwa kama vile maambukizi ya

  • Kirusi cha Rubella

  • Kirusi cha Cytomegalovirus (CMV)

  • Toxoplasmosis

  • Kirusi cha Herpes simplex

  • Kirusi cha Varicella virus

  • Kemikali zinazoliwa kwenye chakula, kupakwa kwenye ngozi n.k



Dalili zingine katika kipindi cha kwanza cha ujauzito kwa wiki

Ili kufahamu dalili na ukuaji wa hatua kwa hatua katika kipindi cha tatu cha ujauzito, bofya makala halisi katika wiki hiyo


Soma kuhusu ujauzito kwa miezi

Majina mengine ya makala hii
  • Miezi mitatu ya kwanza katika ujauzito

  • Traimista ya kwanza

  • Mwezi 1 hadi 3 ya ujauzito


Vipindi vingine vya ujauzito

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

21 Septemba 2024, 09:53:22

Rejea za mada hii:

1. Congenital disorders caused by teratogens. https://bettercare.co.za/learn/congenital-disorders/text/06.html. Imechukuliwa 26.08.2021

2. The First Trimester. https://www.stanfordchildrens.org/en/topic/default?id=first-trimester-85-P01218#. Imechukuliwa 26.08.2021

3. Week-by-Week Pregnancy Calendar. https://kidshealth.org/en/parents/pregnancy-calendar-intro.html#. Imechukuliwa 26.08.2021

4. Josephine R. Fowler, et al. Pregnancy. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK448166/. Imechukuliwa 26.08.2021

5. DEFINITION OF TERATOGENIC DRUGS. https://www.rxlist.com/teratogenic_drugs/definition.htm. Imechukuliwa 26.08.2021

6. Appendix ATeratogens/Prenatal Substance Abuse. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK132176/. Imechukuliwa 26.08.2021

7. TERATOGENS AND THEIR EFFECTS. http://www.columbia.edu/itc/hs/medical/humandev/2004/Chpt23-Teratogens.pdf. Imechukuliwa 26.08.2021

bottom of page