top of page

Vidokezo vya Afya

Kucheza kwa mtoto tumboni

Kucheza kwa mtoto tumboni

Kucheza kwa mtoto tumboni hutokea pale mama anapopata hisia za mtoto kujigeuza, kupiga teke, ngumi au kufanya mjongeo wowote ule unaoleta shinikizo kwenye ukuta wa tumbo la uzazi. Hii ni ishara ya awali ya uzima wa mfumo wa fahamu, mifupa na misuli ya mtoto.

Kukojoa baada ya ngono

Kukojoa baada ya ngono

Kukojoa kwa kutumia nguvu kiasi mara baada ya kushiriki ngono hupunguza hatari ya kupata U.T.I kwa wanawake.

Kulia machozi huondoa homoni zinazoleta msongo mwilini

Kulia machozi huondoa homoni zinazoleta msongo mwilini

Tafiti mbalimbali zinaoyesha kuwa, mtu akilia machozi kutokana na msongo mwilini, machozi yanayotoka hutoa sumu na homoni mbalimbali zinazosababisha msongo mwilini. Homoni za msongo zinapoachiliwa kwenye machozi baada ya kulia husababisha mfumo unaohusika kutuliza mwili ufanye kazi vema na hivyo husababisha kupata tumaini, kufikiria vema na wakati mwingine kupata usingizi mzuri.

Kumsaidia mtoto asinzie haraka

Kumsaidia mtoto asinzie haraka

Ili mwanao asinzie haraka, weka mbali vifaa vya kielektroniki saa moja kabla ya kulala kisha soma au hadithia hadithi nzuri kwa wakati yupo kitandani. Mwanga wa vifaa vya kieletroniki huchochea ubongo ufanye kazi na hivyo kufanya asilale haraka.

Kunyonyesha huku umekunja nne huweza kukufikasha kileleni

Kunyonyesha huku umekunja nne huweza kukufikasha kileleni

Inafahamika kisayansi kuwa, baadhi ya wanawake wanaonyonyesha , mtoto anaponyonya chuchu huamsha hisia kali za kingono zinazoweza kupelekea mama kufika kileleni wakati wa kunyonyesha huku amekunja nne. Hii ni kawaida kifiziolojia, mama anashauriwa kuacha kukunja nne wakati wa kunyonyesha endapo kupatwa na hisia hii inamfanya ajihukumu.

bottom of page