Vidokezo vya Afya

Madhara ya vidonge vya majira
Matumizi ya vidonge vya majira ni njia nyepesi ya uzazi wa mpango inayopendwa na wanawake wengi. Licha ya kuwa na faida nyingi, tafiti zimeonyesha vidonge hivi huongeza hatari ya kupata magonjwa ya fizi na meno, saratani ya titi na shingo ya kizazi, kuganda kwa damu, kuamka kwa kipanda uso na shinikizo la juu la damu. Kama una vihatarishi vingine vya magonjwa haya, ongea na daktari wako akushauri njia nzuri zaidi ya kutumia.

Madini chuma kwa mjamzito
Wakati wa ujauzito, kiwango cha damu hupungua kiasi cha kuhatarisha maisha ya mama na mtoto. Licha ya msisitizo wa kutumia dawa yenye madini chuma ya ziada ili kuongeza damu, epuka kula vyakula vinavyopunguza ufyozwaji wake kama mayai, maziwa na mazao yake, nafaka zisizokobolewa na chai ya kahawa masaa mawili kabla ya kunywa dawa.

Magonjwa 10 yanayoongoza kuua watu Tanzania
Magonjwa 10 yanayoongoza kuua watoto na watu wazima Tanzania ni Malaria, Magonjwa ya mfumo wa chini wa upumuaji, UKIMWI, Upungufu wa damu, Magonjwa ya moyo na misipa ya damu, Majeraha, Saratani, Kusambaa kwa sumu ya bakteria kwenye damu, Madhaifu ya kiuumbaji na Kiharusi. Chukua tahadhari, fahamu kuhusu magonjwa hayo, jifunze na jikinge endapo inawezekana.


