top of page

Vidokezo vya Afya

Uoge maji baridi au moto baada ya mazoezi?

Uoge maji baridi au moto baada ya mazoezi?

Wakati wa mazoezi, mwili huzalisha jasho na kemikali ya laktiki asidi kwa wingi. Ili urejea mazoezi yajayo pasipo maumivu makali, unapaswa kuupoza mwili wako kwa kuoga maji sahihi na wakati sahihi. Je ni maji ya baridi au moto?

Upungufu wa nguvu za kiume: Mwongozo kwa mgonjwa

Upungufu wa nguvu za kiume: Mwongozo kwa mgonjwa

Upungufu wa nguvu za kiume hutokea kwa mwanaume mmoja kati ya watatu. Tatizo hili halimaanishi kuwahi kufika kileleni tu kama wengi wanavyodhani, bali hujumuisha tatizo la ugumba kwa wanaume. Visababishi vingi hutibiwa kwa dawa, ushauri, mbinu mpya za kufanya ngono na tiba saikolojia.

Usifanye ‘dieting’ kupunguza uzito, uepuke ongezeko la uzito mara mbili zaidi ya uliopoteza

Usifanye ‘dieting’ kupunguza uzito, uepuke ongezeko la uzito mara mbili zaidi ya uliopoteza

Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa, asilimia 80 hadi 90 ya watu wanaofanya ‘dieting’, baada ya kupungua na kufikia malengo ya uzito wanaoutaka na kuacha, miili yao hupata ongezeka la uzito mara mbili ya ule ulioupotea kwa kufanya ‘dieting’. Kula vema kila siku kama mbadala wa kufanya ‘dieting’

Usimnyonyeshe mtoto anayepumua kwa shida

Usimnyonyeshe mtoto anayepumua kwa shida

Kupumua haraka haraka kwa mtoto anayenyonya huweza pelekea maziwa kuingia njia ya hewa . Mtoto akipumua haraka haraka au kwa shida, mwache atulie kwanza ndipo umnyonyeshe. Endapo tatizo linaendelea muwahishe hospitali haraka kwa uchunguzi na matibabu.

Usipende kutumia nishati kutoka kwenye vinywaji

Usipende kutumia nishati kutoka kwenye vinywaji

Vinywaji vyenye sukari huwa na nishati nyingi zaidi ya ile inayohitajika na mwili wako. Nishati ya ziada huchangia kupata uzito mkubwa kupita kiasi. Tumia vyakula vigumu kudhibiti uzito na kujikinga na magonjwa mengi.

bottom of page