top of page
Vihatarishi vya kupata kisukari aina ya 2

Vihatarishi vya kupata kisukari aina ya 2-(DM2) ni

 

Imeandikwa na Dr. mangwella sospeter/MD

  • Uzito. Kuwa na uzito mkubwa kunakuweka hatarini kupata kisukari aina ya 2,  jinsi unavyokuwa na mafuta mengi mwilini upinzani katika ufanyaji kazi wa homoni ya insulini huongezeka. Ingawa haina maaana unatakiwa uwe na uzito mkubwa ili upate kisukari ila hata mtu mwembamba anaweza kupata kisukari hiki aina ya 2.

 

  • Maeneo mafuta yalipojihifadhi. Kama mwili wako umehifadhi mafuta sehemu za kuta za tumbo (mwonekano wa kuwa na kitambi) huwa ni kihatarishi cha kupata kisukari zaidi ya mtu mwenye mafuta haya sehemu nyinginezo kama mapaja na nyonga.

 

  • Kutofanya kazi. Kutofanya kazi za Kuushughulisha mwili ili utoe jasho kunaongeza hatari ya kupata kisukari aina ya 2, pia hata wale wanaofanya kazi za ofisini na wakirudi nyumbani hawafanyi mazoezi wanawekwa kwenye kundi hili la kutofanyakazi. Kufanya kazi au mazoezi kunasaidia chembe hai za misuli ya mwili kuongeza utumiaji wa sukari(glukosi) na homini ya insulin.

 

  • Historia ya ugonjwa wa kisukari aina ya 2 kwenye familia- Kama mzazi au watoto wana kisukari aina hii ya 2 basi unakihatarishi cha kupata kisukari katika maisha yako pia.

 

  • Utaifa- Asili ya mtu. Watu weusi-wa Afrika, wa Hispania, wa Marekani, wa Hindi na wa Asia wapo hatarini zaidi kupata kisukari aina ya 2

 

  • Umri. Umri zaidi ya miaka 45 kisukari aina hii ya pili hutokea sana na hii ni kwa sababu labda watu katika umri huu hufanya mazoezi kidogo na pia wanapoteza misuli na kuongezeka uzito sana. Kisukari aina hii kinaongezeka sana kwa vijana wadogo(chini ya umri huu) pia katika karne hizi

 

  • Kisukari wakati wa ujauzito. Kama ulipata kisukari wakati wa ujauzito basi kisukari hicho huweza kuendelea kwa baadhi ya wanawake na endapo umejifungua mtoto zaidi ya kilo 4 basi pia inakuweka hatalini kupata kisukari aina ya 2

 

  • Ugonjwa wa Polycystic ovarian syndrome. Hutokea kwa wanawake , ugonjwa huu husababisha dalili nyingi kama vile kuwa na vipindi vya hedhi katikati ya mzunguko wa hedhi, kuwa na nywele nyingi kama mwanaume(ndevu n.k) na uzito kupita kiasi huongeza hatari ya kupata kisukari aina hii ya 2.

Imeboreshwa 12.03.2020

Rejea

bottom of page