Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella SM, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Dalili Mbaya kwa mama aliyepoteza Ujauzito
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Damu nyingi, homa, maumivu makali, harufu mbaya au kuzimia – hospitali sasa. Soma Damu nyingi baada ya kutoa mimba.
Maelezo
Kawaida
Damu kidogo hadi wastani – hupungua ndani ya siku chache, huweza kudumu hadi wiki 2.
Maumivu kama ya hedhi.
Uchovu, huzuni.
Hedhi kurudi wiki 4–6 – soma Hedhi baada ya kutoa mimba.
Dalili za hatari na maana yake
Damu nyingi, mabonge makubwa – mabaki ya mimba, kizazi kutonywea.
Homa ≥38°C, kutetemeka – maambukizi ya kizazi; huweza kuenea damuni.
Maumivu makali yanayoongezeka – maambukizi, mabaki, au mara chache kizazi kutoboka.
Uchafu wenye harufu, njano-kijani – maambukizi.
Kizunguzungu, kuzimia, moyo kwenda kasi – damu nyingi imepotea.
Maumivu upande mmoja – mimba nje ya kizazi isiyogundulika.
Matiti kuvimba na homa – kwa mimba kubwa, maziwa kujaa au maambukizi.
Huzuni kubwa, mawazo ya kujiumiza – soma Wakati gani huzuni inahitaji msaada.
Nini cha kufanya
Pumzika; kula vizuri, vyakula vyenye chuma.
Usiweke kitu ukeni hadi damu iishe.
Anza uzazi wa mpango – mimba huweza kutungwa ndani ya wiki 2.
Zungumza na mtu unayemwamini kuhusu hisia zako.
Dalili za hatari
Hospitali mara moja ukiwa na:
Kujaza pedi 2 au zaidi kwa saa, saa 2 mfululizo.
Homa na kutetemeka.
Maumivu makali ya tumbo au upande mmoja.
Kuzimia au kizunguzungu kikali.
Mawazo ya kujiumiza.
Lini umwone daktari
Damu kutoka zaidi ya wiki 2 – soma Damu bila mpangilio baada ya mimba kutoka.
Hedhi haijarudi wiki 6–8.
Maumivu ya tumbo yanayoendelea – soma Maumivu baada ya kutoa mimba.
Huzuni zaidi ya wiki 2.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Damu kiasi gani ni nyingi?
Kujaza pedi 2 au zaidi kwa saa, saa 2 mfululizo.
2. Homa baada ya mimba kutoka ni hatari?
Ndiyo; huashiria maambukizi.
3. Damu itakaa siku ngapi?
Kwa kawaida hadi wiki 2, ikipungua taratibu.
4. Harufu mbaya ukeni ni nini?
Mara nyingi maambukizi – kachunguzwe.
5. Nitakamatwa hospitali?
Hapana; PAC ni huduma halali.
6. Huzuni baada ya kupoteza mimba ni kawaida?
Ndiyo, lakini ikizidi au kudumu – tafuta msaada.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:07:19
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
World Health Organization. Abortion care guideline. Geneva: WHO; 2022.
Royal College of Obstetricians and Gynaecologists. Early pregnancy loss: management (with NICE NG126). London: NICE/RCOG; 2019 (updated 2023).
American College of Obstetricians and Gynecologists. Practice Bulletin No. 200: Early pregnancy loss. Obstet Gynecol. 2018;132(5):e197–207.
Ministry of Health Tanzania. National post-abortion care (PAC) guidelines. Dodoma: MoH; 2015.

