top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dr.Sospeter Mangwella, MD

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Erythromycin inatibu nini?

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Hutibu baadhi ya maambukizi ya bakteria ya kifua, ngozi na klamidia; hutumika kama mbadala wa penicillin. Itumike kwa maelekezo tu. Soma Klamidia.



Maelezo


Matumizi (kwa maelekezo)


  • Maambukizi ya kifua na koo kwa wenye mzio wa penicillin.

  • Ngozi – impetigo, chunusi (ya kupaka au kumeza).

  • Klamidia kwa mjamzito au mtoto mchanga, inapopendekezwa na mwongozo.

  • Kifaduro – mbadala wa azithromycin; soma Kifaduro.

  • Mafuta ya macho – kinga kwa kila mtoto mchanga.


Si sahihi


  • Tiba ya H. pylori – hutumia clarithromycin; soma Vidonda vya tumbo.

  • Tiba ya gono – hutumia ceftriaxone; soma Kisonono.

  • Mafua na kikohozi cha virusi – antibayotiki hazisaidii.


Maudhi na tahadhari


  • Kichefuchefu, kutapika, kuharisha, maumivu ya tumbo.

  • Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida – tahadhari kwa wenye ugonjwa wa moyo.

  • Mwingiliano – baadhi ya dawa za moyo, kifafa, warfarin, statins.

  • Mzio – upele, uvimbe.

  • Usugu wa vimelea ni mkubwa kwa matumizi yasiyo sahihi.


Nini cha kufanya


  • Maliza dozi kama ulivyoelekezwa.

  • Mwambie mtoa huduma dawa zote unazotumia.

  • Usinunue antibayotiki bila uchunguzi.


Dalili za hatari


Hospitali mara moja ukiwa na:


  • Uvimbe wa uso, kupumua kwa shida, upele mkubwa.

  • Mapigo ya moyo kwenda kasi au kuzimia.

  • Kuharisha kwa maji mengi au damu.


Lini umwone daktari


  • Hakuna nafuu baada ya siku 3.

  • Kutapika kunakuzuia kumeza dawa.

  • Una mimba au unanyonyesha – kwa ushauri wa dawa sahihi.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Erythromycin inatibu nini?

Baadhi ya maambukizi ya kifua, ngozi na klamidia.

2. Inatibu vidonda vya tumbo?

Hapana; H. pylori hutibiwa kwa clarithromycin pamoja na dawa nyingine.

3. Inatibu gono?

Hapana.

4. Inafaa kwa mjamzito?

Ndiyo, kwa maelekezo, kwa baadhi ya maambukizi.

5. Maudhi yake ni yapi?

Kichefuchefu, kutapika, maumivu ya tumbo.

6. Naweza kuitumia kwa mafua?

Hapana.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 17:08:31

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. World Health Organization. The WHO AWaRe (Access, Watch, Reserve) antibiotic book. Geneva: WHO; 2022.

  2. Workowski KA, et al. Sexually Transmitted Infections Treatment Guidelines, 2021. MMWR Recomm Rep. 2021;70(4):1–187.

  3. Malfertheiner P, et al. Management of Helicobacter pylori infection: the Maastricht VI/Florence consensus report. Gut. 2022;71(9):1724–62.

  4. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

bottom of page