top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dkt. Adolf S, M.D

Dkt. Sospeter B, MD

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Fluconazole katika tiba

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Fluconazole hutibu magonjwa mengi ya fangasi, hasa ya kandida. Kipimo na muda hutegemea ugonjwa – fuata maelekezo ya mtoa huduma.


Maelezo


Magonjwa yanayotibiwa



Maudhi


  • Kichefuchefu, tumbo kuuma, kuharisha, kichwa kuuma.

  • Mara chache – ini kuathirika, vipele vikali, mapigo ya moyo kuvurugika.


Tahadhari


  • Ujauzito – tafiti zimehusisha matumizi ya muda mrefu (na kwa kiasi kidogo hata dozi moja) na hatari ya mimba kuharibika au kasoro; mjamzito mwenye fangasi ukeni hupewa dawa za kupachika ukeni.

  • Mwingiliano – warfarin, baadhi ya dawa za kisukari, presha, kifafa, statins na dawa za moyo; mwambie mtoa huduma.

  • Wenye ugonjwa wa ini au figo – ufuatiliaji.


Nini cha kufanya


  • Tumia kwa ushauri na maliza dawa kama ulivyoelekezwa.

  • Kama fangasi hurudi mara 4 au zaidi kwa mwaka – pima sukari na VVU; soma Hatua kama hujapona fangasi.

  • Kwa fangasi ukeni – vaa chupi za pamba, epuka kusafisha ndani ya uke.


Dalili za hatari


Acha dawa na nenda hospitali mara moja ukiwa na:


  • Vipele vikali, malengelenge, vidonda mdomoni au machoni.

  • Macho kuwa ya njano, mkojo mweusi.

  • Kuzimia au mapigo ya moyo kwenda mbio.


Lini umwone daktari


  • Dalili hazipungui baada ya matibabu.

  • Una mimba au unanyonyesha na unahitaji dawa ya fangasi.

  • Fangasi mdomoni kwa mtu mzima – inaweza kuashiria kinga ya chini.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Fluconazole inatibu fangasi wa ukeni?

Ndiyo, ni mojawapo ya dawa kuu.

2. Mjamzito anaweza kumeza fluconazole?

Haipendekezwi bila ushauri – dawa za kupachika ukeni ni salama zaidi.

3. Fluconazole inatibu fangasi wa kucha?

Ndiyo, lakini inahitaji muda mrefu na ushauri wa mtoa huduma.

4. Naweza kunywa pombe nikitumia fluconazole?

Kwa kiasi kidogo kwa kawaida si tatizo, lakini ini lina kazi zaidi – epuka pombe nyingi.

5. Fangasi imerudi baada ya fluconazole, nifanyeje?

Mwone mtoa huduma; pima sukari na VVU, na huenda ni aina sugu ya fangasi.

6. Mwanaume anaweza kutumia fluconazole?

Ndiyo, kwa fangasi wa uume, ngozi au mdomoni kwa ushauri.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:13

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

  2. Govindarajan A, Bistas KG, Ingold CJ, Aboeed A. Fluconazole. StatPearls. Treasure Island: StatPearls Publishing; 2024.

  3. Mølgaard-Nielsen D, et al. Association between use of oral fluconazole during pregnancy and risk of spontaneous abortion and stillbirth. JAMA. 2016;315(1):58–67.

bottom of page