Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Sospeter B. MD
Dkt Salome A, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Gono huonekana baada ya muda gani?
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Wanaume – siku 2 hadi 7; wanawake mara nyingi hawana dalili. Pima wiki 1 hadi 2 baada ya hatari, hata bila dalili. Soma Kisonono.
Maelezo
Dalili
Wanaume – usaha mzito wa njano/kijani, kuungua ukikojoa, korodani kuuma (mara chache).
Wanawake – ute kuongezeka, kuungua ukikojoa, damu kati ya hedhi au baada ya tendo, maumivu chini ya tumbo.
Koo – mara nyingi kimya; koo kuuma kidogo.
Njia ya haja kubwa – muwasho, usaha, maumivu ya kujisaidia.
Macho – usaha mwingi (pia kwa kichanga wakati wa kuzaliwa).
Vipimo
Kipimo cha usaha au mkojo kituoni.
Tanzania mara nyingi hutibiwa kwa dalili (syndromic) kwa STG.
Pima pia klamidia, VVU na kaswende – soma Klamidia na Muda wa kusubiri kupima.
Nini cha kufanya
Usisubiri dalili – pima ukiwa na hatari.
Matibabu ya STG – ceftriaxone + doxycycline; soma Dawa za gono kwa mwanamke.
Mwenzi atibiwe; hakuna ngono siku 7 baada ya wote kumaliza.
Soma Gono hujirudia?.
Dalili za hatari
Homa na maumivu makali chini ya tumbo, korodani kuvimba ghafla, jointi kuvimba na vipele – kituo cha afya mara moja.
Lini umwone daktari
Usaha au kuungua ukikojoa.
Mwenzi amegundulika na gono.
Tendo bila kinga na mtu ambaye hujui hali yake.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Dalili za gono huanza baada ya siku ngapi?
Kwa wanaume siku 2 hadi 7; wanawake mara nyingi hawana dalili.
2. Naweza kuwa na gono bila dalili?
Ndiyo, hasa wanawake, na kooni.
3. Nipime lini baada ya hatari?
Wiki 1 hadi 2, au mara moja ukiwa na dalili.
4. Gono ya koo ina dalili?
Mara nyingi haina.
5. Mwenzi wangu hana dalili, atibiwe?
Ndiyo.
6. Gono inatibika?
Ndiyo, kwa dawa sahihi za STG.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:51
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.
Workowski KA, et al. Sexually Transmitted Infections Treatment Guidelines, 2021 – Gonococcal infections. MMWR Recomm Rep. 2021;70(4).
World Health Organization. Gonorrhoea (Neisseria gonorrhoeae infection) – fact sheet. Geneva: WHO; 2024.

