Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
31 Oktoba 2026, 15:23:37
Unaweza kukaa kipindi gani ukiwa unashaka kama umepata maambukizi?
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Ndani ya saa 72 – nenda kituo cha afya upate PEP na P2 kama inahitajika. Kisha pima: sasa, wiki 2, na wiki 12 baada ya tukio. Soma Kuonekana kwa HIV kwenye kipimo.
Maelezo
Muda wa kupima kwa kila ugonjwa
VVU – sasa (msingi), na wiki 12 baadaye; soma VVU na UKIMWI.
Kisonono – dalili siku 2 hadi 7; pima baada ya wiki 1 hadi 2; soma Kisonono.
Klamidia – wiki 1 hadi 3; pima baada ya wiki 2; soma Klamidia.
Kaswende – kidonda karibu wiki 3; pima wiki 6 na tena wiki 12; soma Kaswende.
Homa ya ini B – wiki 6 hadi miezi 6; pima sasa na miezi 3 hadi 6; chanjo kama hujachanjwa – soma Homa ya ini.
Herpes – siku 2 hadi 12; hupimwa ukiwa na vidonda; soma Malengelenge ya sehemu za siri.
Trikomona – siku 5 hadi 28.
Nini cha kufanya
Ndani ya saa 72: PEP – soma PEP mara kwa mara; P2 au kitanzi cha shaba ndani ya siku 5.
Tumia kondomu hadi upate majibu ya mwisho.
Mwenzi naye apimwe.
Usinunue antibayotiki 'za kinga' mwenyewe.
Dalili za hatari
Homa, vipele vya mwili mzima, maumivu makali ya tumbo chini au korodani kuvimba – kituo cha afya mara moja.
Lini umwone daktari
Usaha, vidonda, vipele au muwasho sehemu za siri.
Kuungua ukikojoa.
Wasiwasi unaokusumbua – ushauri nasaha unasaidia.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. VVU huonekana kwenye kipimo baada ya muda gani?
Wiki 6 kwa kipimo cha maabara, wiki 12 kwa vipimo vya haraka.
2. Kisonono huonyesha dalili lini?
Siku 2 hadi 7.
3. Kaswende huonekana lini?
Kidonda karibu wiki 3; kipimo wiki 6 hadi 12.
4. Nisubiri dalili kabla ya kupima?
Hapana, wengi hawana dalili.
5. PEP inapatikana muda gani baada ya tukio?
Ndani ya saa 72.
6. Nipime mara ngapi?
Sasa, wiki 2, na wiki 12 – kama mtoa huduma atakavyopanga.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 17:07:17
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.
Workowski KA, et al. Sexually Transmitted Infections Treatment Guidelines, 2021. MMWR Recomm Rep. 2021;70(4).
World Health Organization. Consolidated guidelines on HIV testing services. Geneva: WHO; 2019.

