Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Je, PID inatibika?
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: PID inapona. Anza matibabu mapema, maliza dozi yote, na mwenzi wako atibiwe kabla hamjashiriki tendo tena. Soma PID.
Maelezo
Kwa nini mapema ni muhimu
Kila siku ya kuchelewa huongeza uharibifu wa mirija.
Uharibifu huleta ugumba, mimba nje ya kizazi na maumivu sugu ya nyonga.
Kila PID inayojirudia huongeza hatari zaidi.
Kwa nini PID hujirudia
Kutomaliza dawa – dalili hupotea mapema na wengi huacha.
Mwenzi hakutibiwa – huambukizana upya.
Maambukizi mapya ya zinaa.
Nini cha kufanya
Tumia dawa ulizopewa – soma Dawa za PID na Dawa au dozi kamili ya PID.
Maliza dozi yote hata ukijisikia vizuri.
Mwenzi/wenzi wa miezi 2 iliyopita wapimwe na watibiwe.
Epuka ngono hadi wote mmalize dawa na dalili ziishe.
Pima VVU na kaswende.
Tumia kondomu.
Dalili za hatari
Nenda hospitali mara moja ukiwa na:
Maumivu makali ya tumbo, homa kali, kutapika.
Huwezi kumeza dawa.
Una mimba au hedhi imechelewa.
Hakuna nafuu baada ya siku 3 za dawa.
Lini umwone daktari
PID inajirudia.
Maumivu ya nyonga yanaendelea baada ya matibabu.
Mnatafuta mimba baada ya PID.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. PID inapona kabisa?
Ndiyo, ikitibiwa mapema na kwa usahihi.
2. Nimepona PID, naweza kupata mimba?
Wengi hupata; kama mmejaribu mwaka 1 bila mafanikio, pimeni mirija.
3. Kwa nini PID inarudi?
Kutomaliza dawa, mwenzi kutotibiwa au maambukizi mapya.
4. Mwanaume anaweza kuwa na vimelea vya PID?
Ndiyo, mara nyingi bila dalili – ndiyo maana atibiwe.
5. PID inaleta ugumba?
Inaweza, hasa ikichelewa kutibiwa au ikijirudia.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:07:08
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.
Workowski KA, et al. Sexually Transmitted Infections Treatment Guidelines, 2021 – Pelvic inflammatory disease. MMWR Recomm Rep. 2021;70(4).
World Health Organization. Guidelines for the management of symptomatic sexually transmitted infections. Geneva: WHO; 2021.

