top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Kinyesi cha kwanza cha mtoto hutoka lini?

Jibu kwa ufupi


Swali la mteja: "Mtoto wangu ana siku 2 tangu azaliwe hajatoa kinyesi, ni kawaida?"


Jibu kwa ufupi: Saa 48 bila kinyesi si kawaida – mpeleke kituo cha afya leo. Akiwa anatapika kijani au tumbo limejaa, nenda hospitali mara moja.


Maelezo


Mabadiliko ya kinyesi ya kawaida


  • Siku 1 hadi 2 – mekonium cheusi-kijani, kinachonata.

  • Siku 3 hadi 4 – kinyesi cha mpito, kijani-kahawia.

  • Siku 5 na kuendelea – kwa anayenyonya maziwa ya mama: njano kama haradali, laini, chenye vitone; soma Kinyesi cha kijani kwa mtoto.


Visababishi vya kuchelewa


  • Kunyonya kidogo siku za mwanzo.

  • Kizuizi cha mekonium (meconium plug) – mara nyingi kwa njiti.

  • Hirschsprung – sehemu ya utumbo haina mishipa ya fahamu.

  • Njia ya haja kubwa kutokamilika au kuziba – angalia kama tundu lipo na liko mahali pake.

  • Tezi ya shingo kufanya kazi kidogo, maambukizi ya damu.


Nini cha kufanya


  • Mnyonyeshe mapema (saa ya kwanza) na mara 8 hadi 12 kwa siku – maziwa ya kwanza (dang'a) husaidia mekonium kutoka; soma Namna nzuri ya kunyonyesha.

  • Andika saa ya kinyesi na mkojo wa kwanza na mwambie mtoa huduma.

  • Usimpe dawa za kuharisha, maji, mafuta wala dawa za kienyeji.

  • Usimwingize kitu kwenye njia ya haja kubwa.


Dalili za hatari


Hospitali mara moja ukiona:



Lini umwone daktari


  • Hajatoa kinyesi kufikia saa 48.

  • Hajakojoa kufikia saa 24.

  • Baada ya wiki 1, anatoa kinyesi kigumu kwa shida kila mara.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Mekonium ni nini?

Kinyesi cha kwanza cheusi-kijani cha mtoto mchanga.

2. Mtoto anapaswa kutoa kinyesi cha kwanza lini?

Ndani ya saa 24, na karibu wote ndani ya saa 48.

3. Siku 2 bila kinyesi, nifanyeje?

Mpeleke kituo cha afya leo.

4. Nimpe maji au mafuta kumsaidia?

Hapana; mnyonyeshe mara nyingi.

5. Kinyesi cha mtoto anayenyonya huwa cha rangi gani?

Njano kama haradali, laini.

6. Kutapika kijani kwa mtoto mchanga ni hatari?

Ndiyo, hospitali mara moja.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 17:07:37

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Clark DA. Times of first void and first stool in 500 newborns. Pediatrics. 1977;60(4):457–9.

  2. World Health Organization. WHO recommendations on maternal and newborn care for a positive postnatal experience. Geneva: WHO; 2022.

  3. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

bottom of page