top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Kuchelewa hedhi na kuja mithiri ya vitone vya damu

Jibu kwa ufupi


Swali la mteja: "Hedhi yangu ilipaswa kuanza tarehe 12, lakini tarehe 13 nikaanza kuona vitone vidogo vya damu visivyohitaji pedi. Mpaka sasa sipati hedhi ya kawaida. Shida inaweza kuwa nini?"


Jibu kwa ufupi: Pima mimba kwanza. Kama ni hasi, huenda ni mabadiliko ya homoni ya mwezi huo. Kama ni chanya, nenda kliniki mapema kuhakikisha mimba iko kizazini.


Maelezo


Visababishi


  • Mimba ya mwanzo – damu kidogo wakati kiinitete kinajipandikiza (siku 6 hadi 12 baada ya uovuleshaji).

  • Mimba nje ya kizazi au mimba inayotishia kutoka – vitone pamoja na maumivu.

  • Mabadiliko ya homoni – msongo, ugonjwa, uzito, uovuleshaji kutotokea mwezi huo.

  • Uzazi wa mpango – vidonge, sindano, kipandikizi, P2.

  • Magonjwa ya kizazi – PCOS, faibroidi, endometriosis, polipu.

  • Maambukizi – PID, klamidia, kisonono.

  • Soma pia Damu katikati ya mzunguko.


Nini cha kufanya


  • Pima mimba – kama hedhi imechelewa siku 7 au zaidi; kama hasi na bado haiji, rudia baada ya wiki 1.

  • Andika tarehe za damu kwenye kalenda au programu ya simu.

  • Kama unatumia uzazi wa mpango, mwambie mtoa huduma – inaweza kuwa maudhi ya kawaida.

  • Epuka kumeza dawa za "kuleta hedhi" bila kujua kama una mimba.


Dalili za hatari


Nenda hospitali mara moja ukiwa na:


  • Maumivu makali upande mmoja wa tumbo, maumivu ya bega, kizunguzungu au kuzimia – mimba nje ya kizazi.

  • Damu nyingi ghafla yenye mabonge.

  • Homa na uchafu wenye harufu mbaya.


Lini umwone daktari


  • Vitone vinaendelea zaidi ya wiki 1 au vinajirudia kila mwezi.

  • Kipimo cha mimba ni chanya – kliniki mapema kwa ultrasound.

  • Damu baada ya tendo la ndoa.

  • Hedhi imevurugika miezi 3 mfululizo – soma Hedhi kuchelewa.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Vitone badala ya hedhi ni dalili ya mimba?

Inaweza kuwa. Pima mimba ili ujue.

2. Nimepima mimba ni hasi lakini bado vitone, nifanyeje?

Rudia baada ya wiki 1; vikiendelea, mwone mtoa huduma.

3. Natumia sindano ya uzazi wa mpango na naona vitone, ni kawaida?

Ndiyo, ni maudhi ya kawaida, hasa miezi ya mwanzo.

4. Vitone vya kupandikiza mimba hudumu siku ngapi?

Kwa kawaida siku 1 hadi 3, kidogo sana.

5. Vitone na maumivu upande mmoja ni hatari?

Ndiyo, inaweza kuwa mimba nje ya kizazi – nenda hospitali mara moja.

6. Msongo wa mawazo unaweza kuleta vitone?

Ndiyo, huathiri homoni na kuvuruga hedhi.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:17

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Munro MG, Critchley HOD, Fraser IS. The two FIGO systems for normal and abnormal uterine bleeding symptoms and classification of causes of abnormal uterine bleeding in the reproductive years: 2018 revisions. Int J Gynaecol Obstet. 2018;143(3):393–408.

  2. MSD Manual Professional Version. Abnormal uterine bleeding. Merck & Co.; 2023.

bottom of page